Aende degree ipi kati ya hizi: Civil, Mechanical, Electrical, Mineral au Data Science? Matokeo yake ni GPA 1.6 (PCM)

Maisha ya sasa unaweka lengo usome ili upate ajira? Kwa nini isiwe ''kusoma ili uweze kuendesha maisha''?
 

Mineral na hizi leseni zetu za uchimbaji za magumashi, aachane nayo...Data Science ndiyo mpango mzima...hii ukiisoma na ukaingia kwenye sekta ya FinTech...mbona hata Elon Musk atakuajiri utapiga hela

Elon Musk kawekeza $ 1.5 Trillion katika Data Science kwa miaka 20 ijayo. Fursa hiyo
 
Kati ya Tanzania wenye akili nchi hii ni wewe .Nimekuelewa sana
 
Environment Engineering pia inalipa
 
Data Science, Statistics, Actuarial science zitamfaa, siku hizi kuajiliwa ni bahati, connection na skills & experience tu, asome kitu anachokipenda atafaulu vizuri.
 
Azimio la Musoma. Nimewai kusikia hili azimio lilikua linasema mtu asiende chuo kikuu hadi afanye kazi walau miaka miwili.
Hii ilikua nzuri sana, ilifanya mtu ajitambue, ajitathmini. Akiwa anataka kwenda chuo anajua anaenda kufuata nini.
Sio hii ya mtu anasoma tu afaulu wala hajui anataka nini, ni ajira tu basi
 
Hizo ulizotaja zote hapo ni nzuri. Hapo cha muhimu ni kujua yeye moyoni anataka nini? Ili akichagua moyo wake uridhike huku anasomea kitu anapenda. Aachane na kusoma huku anafikiria atapata ajira au laah...

Kwa ushauri ningempa
1. Mechanical engineering
2. Electrical engineering
3. Civil upande wa buildings....
4. Data science
5. Mineral...
 
Mtu aliyesoma pcm anaweza kuwa tabibu?
 
Ahsante sana mkuu
Ushauri umefika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…