Kenya 2022 Afadhali ya NEC, ile IEBC ni aibu tupu. Tanzania tuko vizuri

Kenya 2022 Afadhali ya NEC, ile IEBC ni aibu tupu. Tanzania tuko vizuri

Kenya 2022 General Election
View attachment 2324674
Hawa makamishna walikuwa wanamuunga mkono odinga…walipendekezwa na uhuru wakaingia kwenye tume ,uhuru aliweka wazi anamsupport raila na hawa aliwapendekeza unadhan walikuwa side gani…
Mwanzo mbona uhakiki ulienda vyema ,gafla mwishon kutangaza ndo wajitoe? Na wafuasi wa raila waanzishe ugomvi nje ya bomas na raila asitokee….hawa wote walitaka kutoa taharuki hawaamin kama ruto kawapiga live…bado walikuwa wanaamin nafasi ya kushinda ipo as walikuwa wanakaribiana sana
Uzuri ni kwamba mahakama imetoa siku 7 za raila kupinga mahakamani kama haridhiki na matokeo na yatachunguzwa upya simple kabisa
Wakapinge mahakamani
Atagaragazwa tu

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Hawa
5778f5db-46bf-4f49-8d16-5f02ce94ab7a.jpg
 
Kama kila kitu kinaenda kwa uwazi na Ukweli kwanini makamishina wa IEBC wanapingana hadharani wenyewe kwa wenyewe?

cc: Halima Mdee na wenzake
Ni Kweli kabisa kule hakuna JECHA Wala MAHELA!!!!

Itatokea huku pia, viongozi wa kifalme watatoswa.
 
Ni wapumbavu pekee wanaweza kusema NEC iko vizuri kuliko IEBC.

Jiulize katika giza la Tanzania wasimamizi kuzuia kupiga hata picha form za matokeo, mawakala kuomdolewa kwenye vyumba vya kuhesabiwa kura, wagombewa kutorusiwa kuingia vyumba vya mawakala, kutoruhusiwa hata kujumlisha kura za mgombea wenu, wagombea kuenguliwa na uchafu wote unaofanyika Tanzania hali ingekuwaje hapo Kenya?

Tatizo la mfumo wa utawala una wajinga wengi na unasupotiwa na wapumbavu wengi ambao hawawezi kutofautisha angaliu hata kati ya zuri na baya.

Mathalani miaka michache iliyopita kuna wapumbavu walisema Tanzania haihitaji katiba mpya ila ndani ya miaka mitano wanasema Tanzania inahitaji katiba. Hili ni kiashiria kwamba uono wa wanasiasa wengi ni mdogo sana. Hawaelewi mahitaji ya wakati uliopo wala mahitaji wa wananchi.

Mapigano yanasababu tofauti na wizi wa kura.
 
Hawa IEBC siyo wakuigwa kabisa wanaeza wakaleta maafa,,, kwanini walisitisha kurusha matokeo live kama kweli walikua sahihi na wanachokifanya!
Fomu zote 46000 zipo mtandaoni mpaka sasa na kila mmoja yuko huru kujumlisha matokeo na kuyahakiki mwenyewe. Shida yenu waliowengi mna uelewa mdogo sana. Sijui kama hii nchi yetu itatoka hapa ilipo kwa mawazo ya namna hii?
 
Kama kila kitu kinaenda kwa uwazi na Ukweli kwanini makamishina wa IEBC wanapingana hadharani wenyewe kwa wenyewe?

cc: Halima Mdee na wenzake
Kila mtu mule Ana maslahi yake na chama chake
Sasa NEC wote ni kijani
Wao kila kitu ndiyooo aka sawa

Ova
 
Back
Top Bottom