Kenya 2022 Afadhali ya NEC, ile IEBC ni aibu tupu. Tanzania tuko vizuri

Kenya 2022 General Election
Atagaragazwa tu

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Kama kila kitu kinaenda kwa uwazi na Ukweli kwanini makamishina wa IEBC wanapingana hadharani wenyewe kwa wenyewe?

cc: Halima Mdee na wenzake
Ni Kweli kabisa kule hakuna JECHA Wala MAHELA!!!!

Itatokea huku pia, viongozi wa kifalme watatoswa.
 
Wakikuyu ndio huamua nani awe rais wa Kenya
 
Ni wapumbavu pekee wanaweza kusema NEC iko vizuri kuliko IEBC.

Jiulize katika giza la Tanzania wasimamizi kuzuia kupiga hata picha form za matokeo, mawakala kuomdolewa kwenye vyumba vya kuhesabiwa kura, wagombewa kutorusiwa kuingia vyumba vya mawakala, kutoruhusiwa hata kujumlisha kura za mgombea wenu, wagombea kuenguliwa na uchafu wote unaofanyika Tanzania hali ingekuwaje hapo Kenya?

Tatizo la mfumo wa utawala una wajinga wengi na unasupotiwa na wapumbavu wengi ambao hawawezi kutofautisha angaliu hata kati ya zuri na baya.

Mathalani miaka michache iliyopita kuna wapumbavu walisema Tanzania haihitaji katiba mpya ila ndani ya miaka mitano wanasema Tanzania inahitaji katiba. Hili ni kiashiria kwamba uono wa wanasiasa wengi ni mdogo sana. Hawaelewi mahitaji ya wakati uliopo wala mahitaji wa wananchi.

Mapigano yanasababu tofauti na wizi wa kura.
 
Hawa IEBC siyo wakuigwa kabisa wanaeza wakaleta maafa,,, kwanini walisitisha kurusha matokeo live kama kweli walikua sahihi na wanachokifanya!
Fomu zote 46000 zipo mtandaoni mpaka sasa na kila mmoja yuko huru kujumlisha matokeo na kuyahakiki mwenyewe. Shida yenu waliowengi mna uelewa mdogo sana. Sijui kama hii nchi yetu itatoka hapa ilipo kwa mawazo ya namna hii?
 
Kama kila kitu kinaenda kwa uwazi na Ukweli kwanini makamishina wa IEBC wanapingana hadharani wenyewe kwa wenyewe?

cc: Halima Mdee na wenzake
Kila mtu mule Ana maslahi yake na chama chake
Sasa NEC wote ni kijani
Wao kila kitu ndiyooo aka sawa

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…