Niliwahi kuishi na wahanga wa vurgu za 1994 Mgusu Geita pale,walikuwa vijana wawili lkn 1994 bado walikuwa watoto wa kati ya 10-13, walikuwa wakisimulia namna walivyochomoka mpaka kuja TZ inastaajabisha sana.
Jamaa anasema alikuwa akitoka kitaa,kufika nyumbani anaona kuna watu wame wazingira wazazi wake,akajificha kichakani huku akichungulia.
Wakamuamlu mama yake amtwange mtoto aliye mgongoni,mama akawa na kigugumizi.
Wakawaingiza na kuipiga nyumba kiberiti 😭😭😭😭
Jamaa aliniambia baada ya kuona vile akakimbia kusiko julikana,ghafla akakuta kuna miili miingi lkn akagundua kuwa wauaji bado wako jirani,akajichanganya humohumo na yeye.
Na kweli,wauaji walikuja kukagua baadae wakasepa. Dogo baadae akachanja mbuga bila kujua anaelekea wapi,ndipo njiani akakutana na makundi ya wahanga wengine,naye akaunga tela mpaka TZ. Hajui nini kiliendelea kwa wazazi wake wala nduguze.
Haya mambo ya vita tuyaepuke sana.