Afande Sele amjia juu Mpoto, adai kutomsema marehemu kumepitwa na wakati

Afande Sele amjia juu Mpoto, adai kutomsema marehemu kumepitwa na wakati

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Sele.jpg

Msanii Afande Sele amesema kitendo cha watu kumwambia kuwa anafanya vibaya kumsema marehemu (Steven Kanumba) ni kitendo ambacho kimepitwa na wakati na mila zisizofaa.

Afande Sele ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, huku akimjibu Mrisho Mpoto baada ya kumwambia anakosea kumsema marehemu kuwa alikuwa anabaka, na kusema kwamba mila kama hizo hazifai kwenye jamii kwani zinaleta madhara makubwa baadaye.

Afande Sele ameendelea kwa kusema kwamba ni ukweli usiopingika kuwa Kanumba alikuwa anafanya dhambi, hivyo ni jambo ambalo halitakiwi kufichwa ili wengine wajifunze kupitia hilo.

Hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa baada ya muigizaji ELizabeth Michael (Lulu) kuhukumiwa kwa kifo cha Kanumba, na baadhi ya watu kusema kuwa alistahili adhabu hiyo huku wenine wakidai ameonewa kwani marehemu alikuwa anamrubuni kutokana na kuwa na umri mdogo kwake.
 
Na mimi narudia, hizi mila za kudai marehemu asisemwe vibaya zimepitwa na wakati. Afande Sele hawezi kutafuta kiki, na wewe unaesema mziki umemshinda utakuwa na maruweruwe, huyu jamaa anamchango mkubwa kwenye Bongo Flavor na kama kuna mtu ataandika kuhusu historia ya huu muziki, basi jina lake litakuwepo.
 
Haileti maana kusubiri mtu afe ndio uongee. Kwa nini usiongee akiwa hai, huoni kama ingemsaidia yeye na wengine wenye tabia hizo?
 
Usitembee juu ya ardhi kwa kuringa.
 
Kutomsema marehemu kumepitwa na wakati.

Lakini pia kujidamkia kusemasema kila jambo bila ya sababu muhimu kwa sababu wewe celebrity tu nako kumepitwa na wakati.

Free country, kila mtu yuko huru kutoa opinion.
 
Free country, kila mtu yuko huru kutoa opinion.
Hata hiyo yangu nayo niko huru.

Freedomof opinion ni kitu kimoja.

Opinion moja kuwa mbaya na nyingine kuwa nzuri ni kitu kingine.

Hakuna ubishi kwamba kila mtu ana uhuru wa kutoa opinion.

Lakini hilo halina maana mtu akisema kula mavi yana faida za kiafya ukubali, kwa sababu ni nchi huru kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni.

Ukweli nikwamba wabongo wengi ni rahisi kutoa ushauri ambao hawajaombwa na wala si lazima kwa mambo wasiyoyajua, wakati wao wenyewe wameshindwa kujiendeleza kwa mambo wanayotakiwa kuyajua.
 
Haileti maana kusubiri mtu afe ndio uongee. Kwa nini usiongee akiwa hai, huoni kama ingemsaidia yeye na wengine wenye tabia hizo?
Kwani kanumba amekufa mwaka 2017 ,si amekufa kitambo ...
 
Back
Top Bottom