Mi nafikiri muziki ni moja ya sanaa ambayo tunaamini inatakiwa kuielimisha jamii,kuikosoa,kuiburudisha na mwisho wa siku kuipa mwongozo katika mambo ya kiuchumi,kisiasa,na kijamii zaidi pamoja na kuwa ajira kwa wasanii.
unaposema/kutengeneza makundi na kuzidisha chuki kwa kutofautiana kimtazamo na unapoendelea kusambaza sumu ya utengano badala ya umoja na maridhiano ni sawa na kushiriki katika kuua sanaa hii,siku zote migongano ya kifikra ni suala lisiloepukika kubwa zaidi mwanaharakati wa kweli ni yule anaetoa hoja yake na kutafuta namna ya kukutanisha pande mbili kinzani na kutafuta suluhu,matusi hayajengi jamani.