Afande Sele: Tarehe 7/7/2026 kulikuwa na Utulivu sio Amani. Tusitamani hii hali ijirudie tena

Afande Sele: Tarehe 7/7/2026 kulikuwa na Utulivu sio Amani. Tusitamani hii hali ijirudie tena

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Msanii wa Bongo Fleva Selemani Msindi(Afande Sele), amesema Tarehe 7/7/2026 kulikuwa na Utulivu sio amani.

Amesisitiza watu wapewe kilichofanya watake kuandamana.

Kasema wanaingiziwa Posho na Mishahara ndo Wanasema kulikuwa na amani. Lakini wanaotegemea miguu ili kula wanasema kulikuwa na Utulivu.

Kasema tusitamani yaliyotokea tarehe 07. 07.2026 yajirudie tena..
 
1783485936645.png
 
Babu ngoma haijaisha hii mambo yakiendelea hivi basi utaanza kuona suicide ama mass murder kwenye maeneo ya umma. Better now than never
Umewaza kama mtu mwenye akili japo waliowengi hawataki kuambiwa ukweli. Hivi wameshasoma chanzo cha watu kujitoa suicide? Au kwanini Haiti au Sudan ya Al Bashir imekuwa vile?

Viongozi uchwara walianza kupokea rushwa na kuongea maneno ya dhiaka wakati Omar Al Bashir anaonywa na ICC wakidai wanamwonea kisa anatokea Afrika. Leo Sudan imetumbukia kwenye vita kisa Al Bashir alijianzishia vikundi vya utekaji na utesaji nje ya mfumo rasmi ya kiutawala.
Wenye kusema tutaendelea kusema ukweli hata ikibidi kupiga hatua za mbele zaidi.
 
Afande sele siku za karibuni amekuwa anapata tabu sana ya kuwashwa kiboga. Sijui dawa yake ni nini?!!!!
 
Hii nchi haina amani hata kidogo, ni hofu tu zimetawala wananchi wengi wakiogopa kudai haki zao kwa hofu ya kuuawa na vyombo vya dola polisi na jeshi ambavyo havilindi tena wananchi bali vinalinda maslahi ya wakubwa wachache wanaojinufaisha na madaraka waliyokwapua kutoka kwa wananchi kwa kutumia vyombo vya dola...

Nakulilia Tanzania
 
Kama haamini katika mungu unaye muamini wewe unataka kumlazimisha !?

Kama haamini katika mungu unaye muamini wewe unataka kumlazimisha !?
Wapi nimeandika nataka kumlazimisha aamini juu ya MUNGU.

Labda kiswahili kimebadilika kwako.
Nimetaka tu kuulizia kama ndiye aliyemtukana MUNGU au siye.

Ungesema ndiye, siye au hujui lolote juu ya tukio hilo ingetosha.
 
Msanii wa Bongo Fleva Selemani Msindi(Afande Sele), amesema Tarehe 7/7/2026 kulikuwa na Utulivu sio amani.

Amesisitiza watu wapewe kilichofanya watake kuandamana.

Kasema wanaingiziwa Posho na Mishahara ndo Wanasema kulikuwa na amani. Lakini wanaotegemea miguu ili kula wanasema kulikuwa na Utulivu.

Kasema tusitamani yaliyotokea tarehe 07. 07.2026 yajirudie tena..
View attachment 3624801
Sijui kama Afande anajua tofauti ya maneno "amani" na "utulivu"
 
Back
Top Bottom