Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Nampongeza kwa uamuzi mzuri.
Kuchomwa moto kutapunguza matumizi ya ardhi kama makaburi, na kuwaachia watu walio hai ardhi waitumie.
Huu ni uamuzi wa kujikana nafsi, kukataa ubinafsi.
Kuna watu walizikwa makaburi ya Tambaza, ikaja kutokea haja ya kupitisha barabara katikati ya makaburi yale, pale Don Bosco kwa juu barabara ya Maliki kati ya Shule ya Msingi Muhimbili na msikiti wa Tambaza.
Kwa kuwa palikuwa na makaburi, na barabara ilihitajika kupita pale, ilibidi makaburi yafukuliwe halafu mabaki ya maiti yazikwe upya, ili kupisha barabara ijengwe.
Kama wale watu wangekuwa wamechomwa moto, kungekuwa hakuna udhia huo.
Nilishawahi kupiga mahesabu na kuona kwamba ikiwa kila mtu atazikwa katika kaburi, kwa miaka 100, dunia nzima itatumia ardhi kama nchi ya Gambia kwa kuzikia watu tu.
Kibaya zaidi, ardhi hii mara nyingi inakuwa karibu na makazi ya watu na inazuiliwa kutumika kwa shughuli nyingine za maendeleo.
Mimi nilishaacha wosia siku nyingi nikifariki nichomwe moto na majivu yangu yatupwe Long Island Sound.