Afande Sele: Wanangu, nikifa mnichome moto

Afande Sele: Wanangu, nikifa mnichome moto

Mkuu binafsi huwa naamini Dunia inarecycle kila kitu kwani binadamu anapozikwa wale worms wanachukua nutrients, energy e.t.c from decaying body ambazo yule binadamu alizokusanya katika maisha yake Yote aliyoishi Duniani na kuzirudisha kwenye udongo ili ardhi ipate rutuba.

Ndio sababu part ya Germany wanazika mtu Kwa miaka ishirini baada ya decomposition ya tissue kuwa imefanyika basi wanafukua mifupa na kuifanyia cremation.

Ni sawa na mfumo mzima upumuaji kati ya binadamu na mmea. Mimea inatoa oxygen kama waste product ambayo kwetu sisi tunahitaji na sisi tunatoa carbon dioxide ambayo mimea inahiitaji.

Nafikiri ni busara sana mtu kuzikwa kwa ajili ya sustainable world's ecosystem.

Its more natural, wild, Free and affordable.

Siku hizi watu wanazikwa kwa kujengewa vijumba kabisa. Yani kaburi inajengeea kijumba kinachodumu zaidi ya miaka 100!

Hata majivu yanakuwa recycled. Ukichomwa moto unakuwa recycled kuanzia dakika unayochomwa moto.

Na hutashikilia ardhi ya mtu hata kwa dakika na kuleta mgogoro wowote kama hao waliozikwa makaburi ya Tambaza.

Kuzikwa au kuchomwa ni haki ya kiutu ya kila mtu na hivyo, kama habari za dini, kila mtu ana uhuru wa kufuata atakavyo.

Ila kuchomwa moto inaondoa unnecessary land use.
 
Sio kosa lako na wala hupaswi kulaumiwa... Nimekujibu ulichouliza kama hujakipenda hainihusu
Kwa hiyo majibu ya swali yanatolewa kwa kuangalia muulizaji atalipenda ama la ?

Duuu ndio maana umeingia kwenye ulozi huku kwengine ungetia aibu endelea kuwaokota huko

Na tufanye ni kosa nani wa kunilaumu humu kwenye ghost Ids ?

Watu Jf sijui mnaichukuliaje
 
Ahahah!! Kumbe siku nyingi umemuona huyu Mshana Jr
Ni aina ya mtu anaye ona makosa ya wenzie ila sasa yeye hataki kuonekana ana makosa ,angekuwa msomi ningesema ana intellectual arrogance sasa huko kwenye Ulozi sijui tunaitaje

Sasa mtu anakuambia ana uhakika Afande Sele atakufa kabla yake ,huyo mtu ni mzima ?
 
Bangi za milimani izo na ukata ndio unamusumbua!!!!.
 
Ni aina ya mtu anaye ona makosa ya wenzie ila sasa yeye hataki kuonekana ana makosa ,angekuwa msomi ningesema ana intellectual arrogance sasa huko kwenye Ulozi sijui tunaitaje

Sasa mtu anakuambia ana uhakika Afande Sele atakufa kabla yake ,huyo mtu ni mzima ?
Nilifikiri ni mimi pekee ninaeona matatizo yake kumbe hata wakongwe kama nyinyi.
 
Itakuwa gharama kubwa naona Kenya wamepiga hatua kubwa sana
Tuna safari kubwa mpaka kufikia hatua ya kuzika kwa njia ya kuchoma miili kwa sababu
. Tamaduni zilizotulea hazina hilo jambo kiasili
. Dini zetu kuu mbili hazijatufundisha kufanya hivyo na hapa zina wafuasi wengi sana
. Bado tuna ardhi kubwa ya kutosha kuzikia
. Bado hatuna maandalizi yoyote ya matanuri ya kuchomea (matanuri ya gesi)

. Hatuna makaburi ya kuhifadhi majivu (mabaki) ambayo yamekaa kama masanduku ya posta

Hii ni mpango mkakati unaohitaji maandalizi mengi sana... Lakini je hili kwasasa ndio kipaumbele chetu?
 
Nampongeza kwa uamuzi mzuri.

Kuchomwa moto kutapunguza matumizi ya ardhi kama makaburi, na kuwaachia watu walio hai ardhi waitumie.

Huu ni uamuzi wa kujikana nafsi, kukataa ubinafsi.

Kuna watu walizikwa makaburi ya Tambaza, ikaja kutokea haja ya kupitisha barabara katikati ya makaburi yale, pale Don Bosco kwa juu barabara ya Maliki kati ya Shule ya Msingi Muhimbili na msikiti wa Tambaza.

Kwa kuwa palikuwa na makaburi, na barabara ilihitajika kupita pale, ilibidi makaburi yafukuliwe halafu mabaki ya maiti yazikwe upya, ili kupisha barabara ijengwe.

Kama wale watu wangekuwa wamechomwa moto, kungekuwa hakuna udhia huo.

Nilishawahi kupiga mahesabu na kuona kwamba ikiwa kila mtu atazikwa katika kaburi, kwa miaka 100, dunia nzima itatumia ardhi kama nchi ya Gambia kwa kuzikia watu tu.

Kibaya zaidi, ardhi hii mara nyingi inakuwa karibu na makazi ya watu na inazuiliwa kutumika kwa shughuli nyingine za maendeleo.

Mimi nilishaacha wosia siku nyingi nikifariki nichomwe moto na majivu yangu yatupwe Long Island Sound.
Teh ...

Hata mimi nimeomba nkifa nchomwe moto !

Ova
 
Tuna safari kubwa mpaka kufikia hatua ya kuzika kwa njia ya kuchoma miili kwa sababu
. Tamaduni zilizotulea hazina hilo jambo kiasili
. Dini zetu kuu mbili hazijatufundisha kufanya hivyo na hapa zina wafuasi wengi sana
. Bado tuna ardhi kubwa ya kutosha kuzikia
. Bado hatuna maandalizi yoyote ya matanuri ya kuchomea (matanuri ya gesi)

. Hatuna makaburi ya kuhifadhi majivu (mabaki) ambayo yamekaa kama masanduku ya posta

Hii ni mpango mkakati unaohitaji maandalizi mengi sana... Lakini je hili kwasasa ndio kipaumbele chetu?
Bado tuna safari ndefu
 
Kwani kuchomwa moto ndiyo Ustaarabu, Mbona hata nchi zilizoebdelea zinamakaburi.

Ukisha kufa umekufa maiti haijui ustaarabu, utupwe bila kuzika, uzikwe, uchomwe moto, ama umwagiwe tindikali uyeyuke. Bado maiti haitambui kinachoendelea.

Hata uwe mstaarabu vipi, ukifia ndani ukiwa unaishi peke yako, watu wasipogundua utaozea kwenye coach ama kitandani.

Ustaarabu utabaki kwa walio hai tu.
Safi, Selemani ni mmoja wa weusi wachache ambao wameshastaarabika, Hana ushamba akilini.
 
Huko hawaharibu mazingira, kwa harufu ya nyama choma ya Binadaam, maana miili mingine hukarbia kuharibika, sijui kama wakati wa kuchomwa panakalika.
Harufu kama tuko mnadani
 
Ugonjwa waakili dalili zake ndio kama hizo.
Huyo jamaa anamatatizo ktk mfumo wake wa akili.
 
Alipaswa kutoa mwongozo kuwa achomweje kwakuwa hata hao wanaochoma kama mabudha, wahindu nk wana dini zao... Na kuna ibada maalum ya mazishi ya kuwachoma marehemu wao.... Nimefanya sana hii kazi
Wasio na dini miili yao hufukiwa ama kutupwa porini iwe chakula cha wanyama....
Asitafute kiki wala kuwapa watoto mzigo wa mawazo
Ana uhakika gani atakufa yeye kabla ya wao
Ana hakika gani atakufa kifo cha maiti yake kupatikana?

Mwisho kama yuko serious anitafute tufunge mkataba nimpe na proforma invoice ya shughuli yote... Nitaifanya hiyo kazi kwa uaminifu na weledi mkubwa
Swahiba ninachoweza kusema kuwa hiyo fursa tayari umeona aandike invoice mfunge mkataba
 
_
Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Afande Sele amewataka watoto wake kwamba akifariki wahakikishe anachomwa moto.
Afande Sele amewataka watoto wake wasimamie hilo kwa kuwa hiyo ni zawadi ambayo anaona itamfaa kutokana na malezi kwa watoto wake hao.
_
Kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii ameadika “Kila wakati nikipata nafasi ya kuongea na hawa binti zangu wawili huwa nawakumbusha kwamba yote ninayowatendea chini ya jua ni wajibu wangu na ni haki yao lakini kitu pekee kikubwa kwangu wanachoweza kunilipa ni wao kuhakikisha kuwa siku yangu ya mwisho ikifika wasiruhusu kivyovyote mwili wangu kuzikwa/kufukiwa udongoni bali zawadi iliyobora kwangu watakayopaswa kunipa ni kuhakikisha mwili wangu unateketezwa kwa Moto na kubakia majivu ambayo ndio watayazika ardhini na kubakia kama alama ya pale nilipo lala mimi ule usingizi mzito na usiokua na ndoto…’maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua’….usifosi tufanane.,” na wasipo fanya hivyo atapita Morogoro yote nyumba hadi nyumba akiwalaani wakazi wote wa huko.
_
Afande Sele awali aliwahi kutoa taarifa ya kutaka asizikwe na achomwe moto huku akidai hana dini hivyo hataki ahusishwe na dini yoyote.

#sourcefb
Aache kabisa na hela ya kuni, sio atusumbue tuu tuliobaki.
 
Back
Top Bottom