Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mwanamke mmoja Mkazi wa Kijiji cha Kanyarakata Kata ya Mbuluma Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa, Albetina Mazwile (42) amefariki baada ya kupigwa fimbo katika sehemu mbalimbali za mwili wake na Mumewe na kupelekea kuvuja damu kwa ndani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale amesema chanzo cha Mume kumpiga Mkewe ni chuki binafsi "Tunamshikilia Mwanaume huyu tukikamilisha uchunguzi tutamfikisha Mahakamani"
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale amesema chanzo cha Mume kumpiga Mkewe ni chuki binafsi "Tunamshikilia Mwanaume huyu tukikamilisha uchunguzi tutamfikisha Mahakamani"
Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limefanikia kumkamata mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa Kijiji cha Kanyalakata, Kata ya Mbuluma wilayani Kalambo kwa tuhuma za kumchapa fimbo mke wake aitwaye Albetina Mazwile (42) na kupelekea kifo chake.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Rukwa, ACP William Mwampaghale amesema mwanaume huyo alianza kumshambulia mkewe kwa fimbo katika maeneo balimbali ya mwili wake na kusababisha kuvuja damu nyingi kwa ndani na baadaye kusababisha mauti.
Anashikiliwa, uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Aidha, ACP Mwampaghale ametoa kutoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za uhalifu ili kukomesha vitendo hivyo.