Afariki baada ya kipigo kutoka kwa mumewe

Afariki baada ya kipigo kutoka kwa mumewe

Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limefanikia kumkamata mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa Kijiji cha Kanyalakata, Kata ya Mbuluma wilayani Kalambo kwa tuhuma za kumchapa fimbo mke wake aitwaye Albetina Mazwile (42) na kupelekea kifo chake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Rukwa, ACP William Mwampaghale amesema mwanaume huyo alianza kumshambulia mkewe kwa fimbo katika maeneo balimbali ya mwili wake na kusababisha kuvuja damu nyingi kwa ndani na baadaye kusababisha mauti.

Anashikiliwa, uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Aidha, ACP Mwampaghale ametoa kutoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za uhalifu ili kukomesha vitendo hivyo.
 
Mwanamke mmoja Mkazi wa Kijiji cha Kanyarakata Kata ya Mbuluma Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa, Albetina Mazwile (42) amefariki baada ya kupigwa fimbo katika sehemu mbalimbali za mwili wake na Mumewe na kupelekea kuvuja damu kwa ndani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale amesema chanzo cha Mume kumpiga Mkewe ni chuki binafsi "Tunamshikilia Mwanaume huyu tukikamilisha uchunguzi tutamfikisha Mahakamani"

Afrika kwa ukatili mhhhh inaongoza!!!!! Kila siku mauwaji, mara kujinyonga/kujiuwa dahhh. Jana wawili wamejinyonga mkoani geita na juzi mmoja.
 
Chuki binafsi ndio nini sasa? Anyway, tubuni na mkamilishe bwawa la Nyerere kama redemption
 
Wanawake nao wamezidi kwa mdomo na masimango tangu..... Wakiuliwa ndio inaonekana wameonewa.

Msipojichunga mtaisha maana stress za field kusaka riziki halafu unafika home mwanamke anakusimanga.....hahahaaa.
Kwa hivyo wanaume hawanaga maudhi kwa wanawake siyo? Na vipi kama mwanamke ndo bread weaner?
 
Miaka 42!? Si mtu mzima huyo? Kweli ni wa kumcharaza viboko?
... hajacharazwa viboko kwa namna unavyofikiria wewe (kama anavyochapwa mtoto); amefanyiwa shambulizi la mwili kwa kutumia fimbo kama silaha; kama fimbo inavyotumika kama silaha kuua nyoka, paka, mbwa, au hata kupambana na vibaka au jambazi lililovamia ghafla.
 
Udhaifu ni kumpiga mwanamke kwa silaha au ngumi,
Yaani wewe ndio unakuwa mwanamke
 
hawa ndio wale wanaume madomo kaya, na nyie wanawake mwisho mwezi huu kuolewa na wanaume wasio jielewa
 
Kuna watu wanajipeleka jela wenyewe tu, tena kwa kutaka.
 
Back
Top Bottom