AFCON 2021| Fixtures, venues, full schedule and kick-off times. Tournament - CAMERON

AFCON 2021| Fixtures, venues, full schedule and kick-off times. Tournament - CAMERON

Bonjour wakuu,

Michuano ya TotalEnergies African Cup of Nations 2021, inategemewa kuanza leo Jumapili 09, Januari 2022.

Michuano hii ilitakiwa ifanyike mwaka jana 2021 ila ilihairishwa kutokana na gonjwa la UVIKO-19 Ila sio wale waliopo bungeni 😂 unaosababishwa na virusi vya Corona. Hivyo CAF ikaamua michuano hiyo ifanyike mwaka huu lakini iendelee na jina lilelile la TATALAFCON 2021.

Pia kutokana na UVIKO-19, timu zitaruhusiwa kuwa na wachezaji 28 badala ya 23 kama ilivyozoeleka.

Vilevile, michuano hii itaandaliwa katika nchi ya CAMERON ambayo kwa Sasa kisoccer inaongozwa na mkongwe Samuel Eto'o Fil. Ambaye kwa namna moja au nyingine ameichangamsha michuano hii kwa kuwazodoa, kuwachamba na kuwapasha wanaobeza, kuponda na kudhihaki michuano hii hasa raia/timu wa/za bara la ulaya ambao walitaka kuwazuia baadhi ya wachezaji wao wasije katika michuano hii mikubwa katika ngazi ya Mataifa, hivyo kuchaguliwa kwake kama raisi wa FECAFOOT mnamo 11 Desemba 2021 imekuwa kama baraka kwa waCameron na waAfrica kuing'arisha michuano hii.

AFCON 2021 groups​

Group A: Cameroon (hosts), Burkina Faso, Cape Verde Islands, Ethiopia
Group B: Guinea, Malawi, Senegal, Zimbabwe
Group C: Comoros Islands, Gabon, Ghana, Morocco
Group D: Egypt, Guinea Bissau, Nigeria, Sudan
Group E: Algeria, Equatorial Guinea, Ivory Coast, Sierra Leone
Group F: Gambia, Mali, Mauritania, Tunisia.

BROADCASTERS
DSTV
-SuperSportpsl
STARTIMES
-World Footbal
AZAMTV
-Utv
-ZBC2

Binafsi timu ninayo shabikia ni Algeria
Timu mbili au moja kati ya hizi mbili zitaingia fainali Senegal &/ Algeria.

Sema chochote, Ongezea lolote , share popote na changia chochote ambacho ni sahihi na chenye staha.
Mbona Taifa Stars siioni?
 
Haya mashindano yananitoa mood yangu ya kuyafatilia baada ya baadhi ya wachezaji kuambiwa wana corona na inabidi wakae ndani
 
Cameroun vs Bukinafaso. Second half ndio imeanza cameroon wanaongoza kwa mabao 2-1.

Bukinabe walitangulia then Cameroon wakasawazisha kwa mkwaju wa penalt kabla ya kupewa mkwaju mwingi wa penalt. Penalt zote kapiga le captain wao.

Nimeshindwa kuelewa kwa nini VAR iliyotoa penalt ya kwanza wametumia picha ya camera moja tu? Hii inaonyesha uwanjani kuna uhaba wa camera.
 
Algeria wanatetea hili kombe. Wachezaji wao ni tofauti na hawa mabishow wa Senegal, Nigeria, Ivory coast na Ghana.
Michezaji yao inayocheza ulaya inajiona mijanjaaah kumbe bure kabisa.
Waarabu ndio wanajua nini cha kufanya yani kazi kazi
 
Back
Top Bottom