Mwamuzi Jan Sikazwe toka Zambia akichezesha mchezo Kati ya Tunisia na Mali, amemaliza mchezo dakika ya 85 lakini Tunisia wakalalamika na mchezo ukaendelea, ilipofika dakika ya 89 akamaliza mchezo tena na safari hii Refa akagoma kuendelea na mchezo.
Mwamuzi huyu amewahi kusimamaishwa kuchezesha soka Kwa miaka 3 alituhumiwa kupokea hongo ili kupanga matokeo.
Hata kama ni ubovu huu wa Leo umepitiliza.
Alianza Kwa kuwanyima Mali Penati DK 58 baada ya Adama Traore kufanyiwa madhambi ndani ya 18 lakini hakutaka hata kujiridhisha Kwa VAR.