Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepangwa Kundi F katika Michuano ya Kombe la Afrika (AFCON) 2023 itakayofanyika Januari 13 hadi Februari 11, 2024 Nchini Ivory Coast na kushirikisha timu 24
Kundi A: Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea, Guinea-Bissau.
Kundi B: Misri, Ghana, Cape Verde, Msumbiji
Kundi C: Senegal, Cameroon, Guinea, The Gambia
Kundi D: Algeria, Burkina Faso, Mauritania, Angola
Kundi E: Tunisia, Mali, Afrika Kusini, Namibia
Kundi F: Morocco, DR Congo, Zambia, Tanzania
Bingwa mtetezi katika michuano hiyo ni Senegal, wakati Misri itaingia uwanjani ikiwa ndio timu inaongoza kwa kulibeba mara nyingi taji hilo, mara 7 ikifuatiwa na Cameroon (5) kisha Ghana (4)