AFCON: Tanzania kumenyana na Morocco, DR Congo na Zambia kundi F

Mpira huu jamani...

Croatia alifika final World Cup 2018 ikumbukwe...
Ha mkuu Croatia imekuwa vizuri enzi na enzi. Usilinganishe mafanikio ya Croatia ni ya muda mfupi mkuu. Mpira no sayansi na sayansi inajengwa kwa muda. Tanzania still has a long way to go
 
Naona hakuna kundi la kifo. Kila kundi Lina m babe mmoja au wawili na vibonde
 
D na E ndo asavali.
 
Wanamichezo kama mnavyofahamu leo ndo inafanzika droo ya upangaji wa makundi ya michuano ya AFCON karibuni tupeane update ya zoezi hilo.
Hivi tulifikaje huku😂😂😂
Naona group zote ni moto kasoro hili la Taifa stars kidogo
 
Taifa Stars ni mafundi wa kupaki bus, kwa Njia hiyo tunatoboa Afcon, Algeria walishindwa kutupasua, hata ije Brazil sijui France hawataweza!

Kinachotakiwa wachezaji wa Taifa Stars wawe na discipline na wasijaribu kujionesha wanajua chenga za kiboya kuonesha wanajua boli huku uwezo mdogo kama zifanyavyo timu ndogo zinapocheza na Simba au Yanga na kupasuliwa!

Kama tumefika Afcon Ina maana tunastahili na tunao uwezo wa kushindana na kutoboa!
 
Ha mkuu Croatia imekuwa vizuri enzi na enzi. Usilinganishe mafanikio ya Croatia ni ya muda mfupi mkuu. Mpira no sayansi na sayansi inajengwa kwa muda. Tanzania still has a long way to go
Sawa huwezi linganisha Tanzania na Croatia, ila katika historia ya mpira Croatia haijawahi kuwa na historia kubwa kupita mataifa ya argentina, Brazil, Italy, Spain, England Belgium, na mataifa mengine makubwa.

Sometimes mpira unachezwa na mentality ya viongozi na wachezaji pamoja na taifa zima kwa ujumla kitu ambacho kinajenga spirit ya wachezaji, ukitizama Croatia ni taifa lenye wachezaji wanaotizamiwa wa viwango vikubwa vya wastani katika ulimwengu wa soka na ni taifa underdog mbele ya magiant nations za kwenye World Cup, kinachoipatia ubora Croatia ni spirit yao ya kulipambania taifa lao ukiangalia mechi zao wachezaji wao wanajitoa wanapambana kwa moyo wote kwaajili ya taifa lao.

Tanzania nayo inaweza kwani kulikuwa na timu bora kuipita Uganda kwa ukanda wa East Africa? Wako wapi leo na Tanzania ipo wapi?
Kuna muda inabidi tukubali kuwa tunaweza na tuache kujidharau, kikubwa tulipende Taifa letu na tuwe na moyo wa kizalendo tusapport timu yetu na sisi, tuache kujiaminisha mambo ya kizamani.

Mpira sio hivyo mnavyoutizama, mpira sio draft kwamba anaejua hafungwi, mpira ni mchezo wa ajabu sana lolote linawezekana kwasababu mpira unadunda.

Tulivyocgeza na Algeria kuna watanzania waliosema tuliachiwa, yani watu hawaipendi timu yao na kukubali maendeleo ya timu ya taifa.

Naiamini Taifa stars na naipenda Tanzania wacha tukafanye wonderful, nyie watanzani waarabu msitukatishe tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…