AFCON (u17)-2017 Gabon: Serengeti boys special thread

Kwa kweli wamejitahdi, ila sapoti bado si ya kutosha yaani madogo wako uwanjani utadhani wao ndio watanzania pekee. Pia hawa vijana wakimaliza mashinda waendelee kuwa kambini kwa ajili ya U20, wakishachukuliwa na yanga na simba basi mpira wao utaishia hapo. Pia vijana washauliwe kufocus mbele si kwa simba na yanga
 

Nyang'au ndio zao😀😀😀😀 Sema wataisoma tu namba
 
Madogo game ya leo wamenifurahisha sana... Ila coacher ashughulikie ile final third yao... Tatzo ni dogo tu yan, ila uwezo wanao.... Viva serenget boys
 
Kwa kweli vijana wanajitahidi, tatizo Watanzania sio wavumilivu. Angola walivyosawazisha matusi yaishaanza. Mpira huo wa kushindaa tuu bila kufungwa duniani haupo. Pia sisi ndio tunashiriki kwa mara ya kwanza, kiwango tu cha uchezaji kitatubeba kwa vijana wetu kuonekana hata tusipofika mbali. Tff toeni hela mpeleke hata mashibiki 500, wenzetu wanaweza sisi tunashindwa nini. Mh Jakaya alishawahi kusema "ukitaka kula sharti uliwe kwanza". Kwa hiyo TFF msitake kula tu
 

Mi mbongo mkuu, nimewaona hao Ghana na niewaringanisha na kikosi chetu, ukweli lazima usemwe timu yetu lazima kache masihara wanapofika kwenye lango la wapinzani, halafu naona kama pasi fupi zinatushinda maana nyingi zinapotea kabla ya kuwafikia walengwa...

Ila kwa leo wamejitahidi japo kwenye banda la mpira nililokuwepo ili kuwa ni kufyonza kwenda mbele na kushangilia mara chache
 
Mali wanalingana pointi na Tanzania lakini wanakaa kileleni kwa 'ustaarabu' wa Alfabeti.
 
Tanzania tunahitaji drop moja kwenda world cup
 
Mali wanalingana pointi na Tanzania lakini wanakaa kileleni kwa 'ustaarabu' wa Alfabeti.


Itakuaje mechi inayofuata mali wakifungwa 3-1. Na sisi tukapotea kwa tatu moja. Atapita nani.?


Nawaza tu, siombei itokee.
 
Niger akishinda 1 - 0 serengeti out.
Kivipi mkuu?
Niger amefunga magoli 3 na amefunga 4, Goal difference yake ni -1.
Tanzania imefunga magoli 2 na imefungwa 1, Goal difference yake ni +1.
Huoni Niger akitushinda 1-0 Goal difference yake itakuwa ni 0 na sisi ni 0?
Au wataangalia nani kashinda tulivyokutana?
 
Itakuaje mechi inayofuata mali wakifungwa 3-1. Na sisi tukapotea kwa tatu moja. Atapita nani.?


Nawaza tu, siombei itokee.
Watapita Niger na Angola kwa Goal difference ya 1 kila mmoja na sisi na Mali tutakuwa na Goal difference ya -1
Labda ungesema Mali wapigwe 2-1 na sisi tupigwe 2-1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…