AFCON (u17)-2017 Gabon: Serengeti boys special thread

Duh wazee wa kupinga pinga mpo. Kuitwa na kujumuika na kiongozi mkubwa wa nchi ni moja ya motisha, kuna mda inabidi tulaumu na kuna mda inabidi tushauri, kwa hapo ilitakuwa kushauri nini kifanyike sio kulaumu.
 
NAHODHA WA SERENGETI BOYS AONDOLEWA KWENYE KIKOSI GABON.

-Nahodha wa timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti boys, Issa Abdi Makamba, hatoweza kushiriki michuano ya AFCON U-17 inayofanyika huko Gabon kutokana na kuumia mguu kulikopelekea kupasuka kwa mfupa wakati akiwa katika moja ya mazoezi kujiandaa na michuano hiyo.

-Kocha wa timu hiyo, Bakari Shime amesema kuwa
" Ni kweli Abdi amepata majeraha hayo ambayo yatamsababisha kushindwa kushiriki michuano hiyo ambapo (leo) Mei 15 Serengeti Boys watamenyana na timu ya Mali"

“Tayari nafasi yake kwa vile tulikuwa na wachezaji wa akiba wameireplace nafasi hiyo. Imekuwa bahati mbaya kwa Issa Abdi mtu ambaye amepambana kwa miaka miwili kuiongoza hii timu kuhakikisha kuwa imefika mahali ilipofika Ataendelea na majukumu mengine kama Captain kuhamasisha..” alisema Shime.

- Aidha madaktari wamesema kuwa Abdi atashindwa kucheza kwa muda wa miezi mitatu ili kuuguza majeraha aliyoyapata katika mguu wake. Kocha huyo aliongeza kuwa kuumia kwa nahodha Abdi, hakutosababisha kushuka kwa kasi waliyonayo vijana wa Serengeti Boys na wanaamini kuwa watafanya vizuri na kupata ushindi katika michuano hiyo.

-Nafasi ya Issa Abdi Makamba anaongezwa kiungo Marco Gerald ambaye alikuwa Gabon kama mchezaji wa akiba
 
[emoji91] MATCHDAY [emoji91]
[emoji460]️ Mali vs Tanzania
[emoji471] [HASHTAG]#CANU17[/HASHTAG]
[emoji625] Stade Sino
[emoji792] 11:30 Jioni (EAT)


Kila la kheri SerengetiBoys
 
Kila la kheri ushindi ni lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…