AFCON (u17)-2017 Gabon: Serengeti boys special thread

AFCON (u17)-2017 Gabon: Serengeti boys special thread

Mkuu serikali inaenda kwa matukio yani hawa vijana waiitiwa wali kwa M/ Rais badala kuitiwa wataalamu wa soko wakubwa duniani kuwapa motivation ya mpira,wewe unamwambia kijana akipata nafasi ya kucheza timu kubwa asisuke nywelee mara sijui nn seriously! yan kama vile tayari kashapata hiyo team.kiukweli tukiacha siasa kwenye mpira tutakuwa mbali sanaa nchi inawatu zaidi ya mil55 lakini hapo Congo kila siku mabomu wanatuzidi mpira,yani viongozi wachache wanatufanya kichwa cha mwendawazimu.
Duh wazee wa kupinga pinga mpo. Kuitwa na kujumuika na kiongozi mkubwa wa nchi ni moja ya motisha, kuna mda inabidi tulaumu na kuna mda inabidi tushauri, kwa hapo ilitakuwa kushauri nini kifanyike sio kulaumu.
 
NAHODHA WA SERENGETI BOYS AONDOLEWA KWENYE KIKOSI GABON.

-Nahodha wa timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti boys, Issa Abdi Makamba, hatoweza kushiriki michuano ya AFCON U-17 inayofanyika huko Gabon kutokana na kuumia mguu kulikopelekea kupasuka kwa mfupa wakati akiwa katika moja ya mazoezi kujiandaa na michuano hiyo.

-Kocha wa timu hiyo, Bakari Shime amesema kuwa
" Ni kweli Abdi amepata majeraha hayo ambayo yatamsababisha kushindwa kushiriki michuano hiyo ambapo (leo) Mei 15 Serengeti Boys watamenyana na timu ya Mali"

“Tayari nafasi yake kwa vile tulikuwa na wachezaji wa akiba wameireplace nafasi hiyo. Imekuwa bahati mbaya kwa Issa Abdi mtu ambaye amepambana kwa miaka miwili kuiongoza hii timu kuhakikisha kuwa imefika mahali ilipofika Ataendelea na majukumu mengine kama Captain kuhamasisha..” alisema Shime.

- Aidha madaktari wamesema kuwa Abdi atashindwa kucheza kwa muda wa miezi mitatu ili kuuguza majeraha aliyoyapata katika mguu wake. Kocha huyo aliongeza kuwa kuumia kwa nahodha Abdi, hakutosababisha kushuka kwa kasi waliyonayo vijana wa Serengeti Boys na wanaamini kuwa watafanya vizuri na kupata ushindi katika michuano hiyo.

-Nafasi ya Issa Abdi Makamba anaongezwa kiungo Marco Gerald ambaye alikuwa Gabon kama mchezaji wa akiba
e9cd2779c1e3f2d64ffc7e1e2fb19ea0.jpg
 
[emoji91] MATCHDAY [emoji91]
[emoji460]️ Mali vs Tanzania
[emoji471] [HASHTAG]#CANU17[/HASHTAG]
[emoji625] Stade Sino
[emoji792] 11:30 Jioni (EAT)
22e41420a8ceeed5e3395d9ef9d7278c.jpg
f9f4e9c58ad55e0c1c1409be53166f1a.jpg


Kila la kheri SerengetiBoys
 
Back
Top Bottom