Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. Akinwumi Adesina amesema kwenye mkutano wa mwaka wa benki hiyo uliofanyika tarehe 24 mwezi huu huko Accra, Ghana kuwa benki hiyo itakusanya dola bilioni 25 za kimarekani kabla ya mwaka wa 2025 kwa ajili ya kuunga mkono nchi za Afrika kwenye juhudi zao za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yameathiri vibaya bara hilo na kusababisha majanga mengi ya asili kama vile ukame, vimbunga na mafuriko. Hasara za kiuchumi zilizosababishwa na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika zinaweza kufikia dola za kimarekani bilioni 7 hadi bilioni 15 kila mwaka.