Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Kupitia vyombo vya habari Kundi la Taliban linaloongoza Serikali ya Afghanistan limepiga marufuku Binadamu na Wanyama kuonekana kwenye Televisheni katika maudhui ya aina yoyote kuanzia Matangazo ya Taarifa ya Habari na burudani nyinginezo na badala yake vioneshwe vitu kama majengo, magari na miti, na vitu vinginevyo, Sauti tu ya mtangazaji ndio isikike ikitangaza ila binadamu anayetangaza hasionekane wala mnyama wa aina yoyote kuonekana kwenye luninga.
Taliban wamesema sheria hiyo inatokana na maandiko ya kiislamu yanayojulikana kama "Sharia Law". Taliban waliongeza kuwa picha za wanyama na sura za watu kwenye Televisheni utumika kwenye Siasa za Ulaya na Marekani. Hivyo ni marufuku Televisheni kuonesha sura na umbo la binadamu na mnyama kwenye Televisheni.
Maafisa wa serikali hawatakiwi kuonekana kwenye Televisheni wakati wa kutoa hotuba au maelezo, sauti zao tu ndio zisikike.
Baadhi ya Waafaghan wamepinga hatua hiyo na kusema unaminya uhuru wa kutoa habari ususani za mahojiano.