Afisa LATRA aliemtishia dereva lori panga asimamishwa kazi (+video)

Afisa LATRA aliemtishia dereva lori panga asimamishwa kazi (+video)

Pascal_TZA

Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
27
Reaction score
76
Mamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini LATRA imemsimamisha kazi Afisa wake kutoka Mkoa wa Lindi ambaye video yake imesambaa mtandaoni akimshikia silaha aina ya panga dereva wa lori lenye namba ya usajili T412 DNN kilichotokea tarehe 11/11/2020.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema sasa kinachoendelea ni uchunguzi wa tukio hilo na adhabu kali zitachukuliwa kwa muhusika ndani ya siku 21 za uchunguzi kulingana na sheria za utumishi wa umma.

"Hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria dhidi ya Afisa huyo zinaendelea kuchukuliwa na hatua ya kumsimamisha kazi imechukuliwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2003 ya utumishi wa umma" Mkurugenzi Mkuu LATRA

Pia soma > Lindi: Mtumishi wa LATRA amtishia sime dereva wa lori ili ampe leseni

 
Hata alochukua video kwa matakwa yake binafsi bila ridhaa "consent" ya walokuwa wanarekodiwa nae ametenda kosa kisheria ....na alorusha pichaa....hahaaaa mnyororo wa makosa

ila mida mingine inasaidia kufichua maovu
 
Inanilillah wa innalilah rajun
Pamoja na kuwa mimi ni KAFIRI (kwa mujibu WAO) na hayo maneno sijui maana yake, lakini huwa nayasoma au kuyasikia pale zinapotolewa salamu za TANZIA. Sasa, sijajua kwa habari hii, hayo maneno yana maana gani?
 
Masikini anajuutraaaa Saiv Huko aliko wakati huo dreva anakula bia banana na wenzake
Kama mimi mtu mmeombana msamaha halafu unanikomalia lazima nikuendee Ngende au Bagamoyo nikupige jini makata
 
Pamoja na kuwa mimi ni KAFIRI (kwa mujibu WAO) na hayo maneno sijui maana yake, lakini huwa nayasoma au kuyasikia pale zinapotolewa salamu za TANZIA. Sasa, sijajua kwa habari hii, hayo maneno yana maana gani?


Hapana maneno haya hutamkwa kwenye msiba. Na msiba au ajali au janga si lazima mtu afe. Kwenye aya ya nyuma yake imetaja baadhi ya majaribu ambayo mja akijaribiwa hutamka maneno haya...

2:155. Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri,

2:156. Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea
 
Mfukuzeni kazi ili msomi mmoja apate hiyo nafasi
Good job Bw. Mkurugenzi
Si mpaka wakujue na ujulikane..watu walihudhuria mazishi asubuhi kwenda ofisini wakaambiwa nafasi imeshajazwa tayari..mjini hakufahi
 
Good decision Tanzania kuna wataalamu wenye nidhamu zaidi ya milioni 2. Fukuza huyo mjinga weka wenye nidhamu period.
Kuna wale wa manispaa pia mmhh zero brain wengi sana aisee
 
Back
Top Bottom