KERO Afisa Maendeleo ya Jamii wa Pangani ni kikwazo cha kuinuka kwa vikundi vya 10%

KERO Afisa Maendeleo ya Jamii wa Pangani ni kikwazo cha kuinuka kwa vikundi vya 10%

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi wanakikundi tuliomba mkopo wa Halmashauri na tukafanikiwa kukopeshwa shilingi milioni tano kwa ajili ya mradi wa mama lishe, tulifuata taratibu zote za kuhudhuria mafunzo, kusaini mikataba ya kurejesha fedha hizo baada ya fedha kuingizwa kwenye akaunti ya kikundi tumezuiwa kuitoa bila ya sababu zinazoeleweka.

Muda wa marejesho unakaribia hatujui tutafanyaje maana huyu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya amekuwa akitutolea kauli chafu pale tunapofuatilia kutoa fedha hizo.

Baada ya kuuliza vikundi vingine vilivyopata mikopo navyo vinalalamika inaonekana mpaka wengine imewalazimu kumshawishi kuwa wakitoa fedha hizo watampa kiasi fulani cha fedha ndipo anawaruhusu kutoa fedha hizo ili apewe gawio.

Nimefuatilia baadhi ya vikundi vinavyolalamika ni Amkeni, Kikundi cha Wanawake kipo Mkwaja, Mshikamano B Kikundi cha wanawake kipo Kipumbwi, Tupendane kikundi cha vijana kipo Kipumbwi, Ngekewa kikundi cha vijana kipo Mwera (hawa ilibidi watoe fedha ili waruhusiwe kutoa fedha ya mkopo).

Vingine ni kikundi cha Amkeni kipo Bweni, kikundi cha Jeshi la mama kipo Pangani Magharibi.

Tunaomba mtusaidie viongozi, huu mkopo umekuwa ni changamoto kila siku ni kupoteza nauli kutoka Kata ya Mkwaja mpaka Pangani kufuatilia fedha hizo ila Afisa Maendeleo Jamii hataki kutusainia tutoe.

Tukumbuke Serikali imejitahidi kuwawezesha wananchi ila huyu mtumishi amekuwa kikwazo kwa ukuaji wetu.
 
Back
Top Bottom