Afisa maudhui CHADEMA kizimbani

Afisa maudhui CHADEMA kizimbani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Afisa Maudhui wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dominic Mgaya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kosa la kuchapisha maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

1600496375653.png

Akisoma hati ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo RIchard Kabate, wakili wa Serikali, Adolf Ulaya amesema kuwa mshitakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 127 ya mwaka 2020.

EFB5D0BE-69E6-47B0-B0C5-A940E1EADF02.jpeg

Mgaya anadaiwa kurusha maudhui kupitia ukurasa wa YouTube wa CHADEMA MEDIA TV bila kuwa na leseni ya mamlaka husika, kati ya Oktoba 14, 2017 na Septemba mosi, 2020 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Aidha, mshitakiwa amekana kutenda kosa hilo na amefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana kama ilivyoamriwa na Mahakama.

Hata hivyo upande wa mashitaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 20, 2020 itakapotajwa.
 
chadema mkichukua nchi mtafuta TCRA?
Hapana sidhani kama watafuta ila walew watendaji wanaowahisi ni waovu watafutika katika ajira kama utakavyoona baadhi ya viongozi/watumishi wakubwa wa majeshi mahakama na kadhalika!na si kwamba watafukuzwa kazi bali madaraka yao yatatenguliwa watatafutiwa kazi nyi ginew kama watakuwa hawana jinai yeyote.
All in all wana kila sababu ya kukibeba ccm maana it is their life line
 
sasa ruzuka mil 300 kila mwezi, bado wanachama wanachanga! bado wananchi wanachanga! leseni mil 1.3 kwa miaka mitatu, whats going on chadema

Sasa si bora hata ya hao wanao changishana kwa hiyari! Nyinyi mnajikombea tu kwenye taasisi na mashirika ya umma bila hata ya aibu!

Mbaya zaidi hela zote mnawahonga wasanii ili tu kuvutia halaiki ya kuhudhuria mikutano yenu.
 
sasa si bora sisi matumizi ya pesa yanaonekana, nyie je?
 
Kwa hiyo huoni hiyo michango inavyo mnyoosha mgombea wenu kiasi cha kumfanya kukata pumzi mara kwa mara?

hio pumzi mnayoongelea mngejua ndo hali yenu, mwenzako lema ashajua hakuna future chadema: kwenye mikutano yake watu wanakuja wamevaa ccm na bado anawakaribisha waombe kura! mmebaki tu nyie na lissu wenu
 
Afisa Maudhui wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dominic Mgaya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kosa la kuchapisha maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

View attachment 1574006
Akisoma hati ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo RIchard Kabate, wakili wa Serikali, Adolf Ulaya amesema kuwa mshitakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 127 ya mwaka 2020.

Mgaya anadaiwa kurusha maudhui kupitia ukurasa wa YouTube wa CHADEMA MEDIA TV bila kuwa na leseni ya mamlaka husika, kati ya Oktoba 14, 2017 na Septemba mosi, 2020 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Aidha, mshitakiwa amekana kutenda kosa hilo na amefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana kama ilivyoamriwa na Mahakama.

Hata hivyo upande wa mashitaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 20, 2020 itakapotajwa.
Aiseee...[emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Sipendi hii tabia ya kumburuta mtu mahakamani halafu unadai ushahidi haujakamilika? Kwa nini usisubiri ukamilike, umshitaki na kuiachia mahakama itoe hukumu? Kupotezeana muda tu.
 
Back
Top Bottom