GE2025 Afisa Mawasiliano CHADEMA Brenda Rupia adaiwa kukamatwa na Jeshi La Polisi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ukiona Gen Z wa kenya wanaamua kupambana jino kwa jino na polisi ujue ni uluuzi kama huu.... Wtz tumekuwa waoga kupitiliza.... Roho ya kikatili waliyonayo viongozi matahira kama sa100 inapswa tuivae na sisi tupigane mkono.
 
Mkuu hizi jeuri zako ni za muda tu. Try to be humble. Uwe na utu na ubinadamu.
Waambieni waache kuwasumbua wanachama wao wa jinsia ya kike,haki za binadamu zinapinga Hilo,akina Baltazari Engonga wapo wengi CDM
 
Nikikumbuka Yale maamdishi katika hati ya kusafiria a.k.a passport,sishangai hili
 
SATIVA17
@Sativa255
TAARIFA KWA UMMA

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA
@BrendaRupia
amekamatwa na maofisa wa Uhamiaji akiwa ofisi za Uhamiaji katika mpaka wa Namanga wakati anafanya process ili aweze kusafari kuelekea nchini Kenya.

Maofisa wa Uhamiaji wanasema kwamba wamepewa maelekezo kwamba Viongozi wa CHADEMA hawatakiwi kutoka njee ya mipaka ya Tanzania so wamemnyang'anya passport yake.

Muda huu Maofisa wa Uhamiaji wamemkabidhi Brenda kwenye mikono ya Jeshi la Polisi kwa OCCID wa Namanga na sasa wanataka kumsafirisha kinyemela kumpeleka Dar es salaam.
 
View attachment 3403542

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Brenda Rupia anadaiwa kushikiliwa na Polisi mkoani Arusha.

Ujumbe wa X uliotumwa na Makamu wa CHADEMA, John Heche leo, umesema kuwa bado wanafuatilia suala hilo.
Kuna watu hawana akili kabisa, unaacha kualika pisi hii kali kabisa upate nayo lunch, unaweka mahabusu!
 
Vyombo vyenye mamlaka ya kukamata Tz:
1)Polisi
2)Uhamiaji
3)Usalama wa Taifa

Tena afisa Uhamiaji anakukamata, kukupekua bila warranty awe Mgeni au Mtanzania
 
Mtu mwenyewe ana akili za kimalaya kila wakati kuwaza atapinduliwa Kwa mume wake mnafikiri atafanya Nini!!
 
Samia na genge lake la mafisadi na majizi yameamua jujimilikisha tanganyika kwa kutumia mabavu. Naona mwisho wake ukiwa kama ule wa jpm, ni swala la mda tu
 
Uhuru uko wapi sasa kama watu wanazuiwa kusafiri ilihali hakuna zuio lolote la kisheria dhidi yao zaidi ya umafia wa gizani, aisee.

Tafrisi yake Kuna watu wamewekwa kizuizini bila ya wao kujitambua.

ndani ya viunga vya Basra -Iraq.
 
Huu uonevu hata shetani hawezi kuvumilia. Cdm wabadili strategy vinginevyo uonevu ni furaha na mafanikio yao watesaji wao.

Walianza na Naibu katibu na sasa kilamtu mwenye influence
 
Duh, sasa kwa unyanyasaji kama huu tusemeje? Huu mbona ni ubaguzi?
 
Kwa nn chadema wasiende mahakamani kupinga huu uonevu wa wazi kinyume na katiba? Je uhamiaji ni ya ccm au. Watanzania wote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…