Afisa Mtendaji wa mtaa wa Mbezi Msumi ashambuliwa hadi kufa ofisini kwake

Afisa Mtendaji wa mtaa wa Mbezi Msumi ashambuliwa hadi kufa ofisini kwake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
MAUAJI ya kutisha yametokea eneo la Mbezi Msumi mkoani Dar es Salaam baada ya watu wasiofahamika kudaiwa kuvamia ofisi za Serikali ya Mtaa wa eneo hilo na kisha kumuua Ofisa Mtendaji kwa kumkata na panga.

Tukio hilo la mauaji limetokea leo Oktoba 11, 2021 kati ya saa sita hadi saa saba mchana wa leo na inadaiwa ofisa huyo mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Msumi ameshambuliwa kwa kukatwa na panga shingoni na watu ambao hawahamiki.

Akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog leo Mmoja wa mashuhuda na mwananchi wa eneo hilo(jina limehifadhiwa) amedai wameshangazwa na tukio hilo la mauaji ambalo limefanywa kwa kiongozi huyo.

Alipoulizwa iwapo watu waliofanya tukio wamefahamika, amejibu hawajafahamika kwani baada ya kutekeleza unyama huo walikimbia na haijulikani ni akina nani na wametoka wapi, ingawa anaamini Jeshi la Polisi linajua namna ya kufuatilia tukio hilo na kuupata ukweli.

"Wananchi tumejawa na taharuki baada ya kutokea tukio hili la mauaji , hatuji nini kimesababisha hadi watu hao kufanya unyama huu kwa kiongozi wa Serikali ya Mtaa,tupo hapa tunasubiri kuona nini kinachoendelea,"amesema shuhuda huyo alipokuwa akizungumza na Michuzi TV

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Ramadhan Kingai aliyezungumza na Michuzi TV amethibitisha kupata taarifa hizo za tukio la mauaji na tayari askari polisi tayari wako eneo la tukio."Tumepata taarifa za tukio hilo,tunafuatilia na baadae tutatoa taaria rasmi kwa vyombo vya habari."

Michuzi TV na Michuzi Blog inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa karibu ili kuhakikisha umma wa Watanzania unafahamu ukweli wa tukio hilo kupitia Jeshi la Polisi ambalo limeanza kufuatilia.
 
Ulinzi shirikishi wameshindwa kumuokoa afisa mtendaji..
 
"..na Kwa sababu ya kuongezeka maasi,upendo wa wengi utapoa" Mathayo 24:12

Siku hizi kosa linaweza kuwa dogo sn lkn solution wanayoona ni kumwomdolea mtu uhai..binadamu amekuwa kiumbe katili Sana

Juzi mtoto kamuua mamaake temeke,kanda ya ziwa jamaa kamuua aliyetembea na mamaake,sasa sijui anataka mamaake akapumzike wapi,unamwekeaje wivu mamaako,mwingine kamuua mkewe mbele ya mtendaji wa kijiji..nchi ngumu sn hii asee

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Pole kwa wafiwa.

Uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini sababu za mauaaji.

Tuwe macho na wale wote ambao mara zote husababisha fujo na kutaka kuhatarisha amani ya nchi yetu.

Magenge ya kihuni yachunguzwe.
 
Kuna jamaaa yangu aliniambiaga kazi za afisa mtendaji zipo kisiasa.
 
Back
Top Bottom