Pre GE2025 Afisa Uandikishaji Halmashauri ya Mbeya: Msilewe na kutumia vilevi wakati mnaandikisha wananchi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Waandishi wasaidizi na waongozaji mashine za biometric (BVR) kwenye zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya, wametakiwa kutotumia vinywaji vyenye vilevi wakati wa zoezi la kuboresha Daftari la mpiga kura linalotarajiwa kuanza Desemba 27, 2024 hadi Januari 2, 2025.
IMG_1972.jpeg

Wito huo umetolewa na Afisa Uandikishaji wa halmashauri ya Mbeya jimbo la Mbeya Vijijini, Gidion Mapunda kwenye mafunzo kwa waandishi hao na wasimamizi wa vifaa vya BVR.

Aidha, Mapunda amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa weledi katika utekelezaji wa zoezi hilo na kuwaasa kwenda kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu.

Pia, amewasisitiza kuepuka matumizi ya vilevi ili kuhakikisha kazi ya uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura inafanyika kwa ufanisi mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.
IMG_1973.jpeg

Kwa upande wake, Afisa msaidizi wa uchaguzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Mwalimu Martin Kija amesema kuna vituo 322 vya uboreshaji vilivyotengwa katika kata 28 za halmashauri hiyo.

Kija amewataka wananchi kuhakikisha wanajiandikisha katika kituo kimoja tu na kuepuka tabia ya kujiandikisha mara mbili.
IMG_1974.jpeg

Nao baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo akiwemo Mpuniza Sanga na Filibart Mtenzi wameeleza kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuahidi kwenda kufanya kazi kwa bidii na kufuata maadili ya kazi katika vituo watakavyopangiwa.
IMG_1975.jpeg

Ikumbukwe kuwa uboreshaji wa Daftari la mpiga kura ni maandalizi muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo wananchi watachagua Madiwani, Wabunge na Rais, hivyo jamii inaaswa kwenda kujiandikisha na kuhuisha taarifa zao ili kupata kadi ya mpiga kura.
 
Wakuu,

Waandishi wasaidizi na waongozaji mashine za biometric (BVR) kwenye zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya, wametakiwa kutotumia vinywaji vyenye vilevi wakati wa zoezi la kuboresha Daftari la mpiga kura linalotarajiwa kuanza Desemba 27, 2024 hadi Januari 2, 2025.

Wito huo umetolewa na Afisa Uandikishaji wa halmashauri ya Mbeya jimbo la Mbeya Vijijini, Gidion Mapunda kwenye mafunzo kwa waandishi hao na wasimamizi wa vifaa vya BVR.

Aidha, Mapunda amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa weledi katika utekelezaji wa zoezi hilo na kuwaasa kwenda kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu.

Pia, amewasisitiza kuepuka matumizi ya vilevi ili kuhakikisha kazi ya uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura inafanyika kwa ufanisi mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake, Afisa msaidizi wa uchaguzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Mwalimu Martin Kija amesema kuna vituo 322 vya uboreshaji vilivyotengwa katika kata 28 za halmashauri hiyo.

Kija amewataka wananchi kuhakikisha wanajiandikisha katika kituo kimoja tu na kuepuka tabia ya kujiandikisha mara mbili.

Ikumbukwe kuwa uboreshaji wa Daftari la mpiga kura ni maandalizi muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo wananchi watachagua Madiwani, Wabunge na Rais, hivyo jamii inaaswa kwenda kujiandikisha na kuhuisha taarifa zao ili kupata kadi ya mpiga kura.

1735034321752.jpeg
 
Back
Top Bottom