Nipo hapa kwenye foleni mwanza nimempa lift mwanamke mmoja sasa nasikia anaongelea hayo mauaji kwenye simu. Na siwezi kumuuliza.
Ila kwa anavyoongea inaonekana huyo mwanamke alikua anatongoza wanawake wenzie na anajulikana hadharani. Na inasemekana kauliwa na kukatwa mkono.
Wenye taarifa kamili tujulisheni.
Nawasilisha.
======
UPDATE;
POLISI YATHIBITISHA KUTOKEA KWA MAUAJI
Akizungumzia kuhusu taarifa hizo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Berthaneema Mlay amesema “Ni kweli tukio hilo limetokea, marehemu ametambulika kwa jina la Milembe Suleiman alikuwa mfanyakazi wa GGM, kitengo cha Ugavi amekutwa ameuawa katika eneo ambalo anajenga nyumba zake.
Eneo ambapo tukio limetokea linaitwa Mwatulole ambazo zilikuwa katika hatua ya ujenzi, mpaka sasa wameshikiliwa watu wanne na uchunguzi unaendelea.”
Alipotakiwa kuelezea kuhusu uchunguzi wa awali wa tuko hilo amesema “Yaani hatujabaini chochote mpaka sasa, ndio maana uchunguzi unaendelea.”
Pia soma
--
Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa watatu waliofanya mauaji ya mfanyakazi mmoja wa Mgodi wa GGM kwa jina la Milembe Selemani katika mtaa wa Matulole, Kata ya Buhalahala mkoani Geita. Aidha Mtuhumiwa wa nne (Pastory Lugodisha), baada ya kupata taarifa ya kukamatwa kwa wahalifu wenzake...
www.jamiiforums.com