Africa Cup of Nations (AFCON) 2015 updates

Nilikuwa nasapoti south afrika Na DRC lakini sio mbaya ivory coast wamechukua ingawa kimpira ghana walicheza vizuri zaidi
 
Bye, tunaonana Libya 2017 Mungu akipenda, Shukrani nyingi kwa Equatorial Guinnea kwa kuokoa mashindano.

Kama sikosei Libya alipokwa kuandaa hizo fainali...

Nakumbuka kina Jamal walifanya mpango wa kuomba hiyo nafasi wakatoswa...

Sijajua nchi gani imepewa nafasi sasa.
 
Mi nina wasiwasi yule kipa kapokea mlungula.

Yule si kipa wa kucheza mashindano yale, nashangaa kwanin kocha hakumpanga dauda huenda angebahatisha kudokonyoa moja. Razack ameimaliza Ghana.
 
Masuke uwe na huruma kidogo..hiki kizazi cha Ivory Coast kingeisha bila kubeba hili kombe ingekuwa jambo la kusikitisha sana kwenye historia zao, namuonea huruma Drogba pia.

Atleast vijana wa Ghana bado wana muda wa kurudia tena.

Hawa Ivory Coast ni uzembe wao wenyewe 2006 na 2012 ilikuwa halali yao kabisa hasa 2012 maana Zambia haikuwa timu nzuri sana, Nakumbuka 2006 tuko hall four, chumbani tulikuwa watu kama kumi hivi, karibu watu wote walikuwa Ivory Coast isipokuwa mimi na Ras tukaamua kuwashabikia Misri na mwishoni sisi wawili ndo tukafurahi.

Labda Ivory Coast hawana bahati na majina ya Didier maana Didier Drogba na Didier Zokora wamestaafu halafu jamaa ndo wakaja kubeba. Hongera zao sana na leo bahati ilikuwa kwao, unakumbuka zile mbili zilizogonga mwamba?
 
Umenikumbusha mbali..

Ni kweli hawa jamaa gundu limewasumbua sana, atleast akina Toure leo wanacheka.
 
Bye, tunaonana Libya 2017 Mungu akipenda, Shukrani nyingi kwa Equatorial Guinnea kwa kuokoa mashindano.

2017 sio mbali, na sisi lazima twende na timu yetu Taifa Stars, penalty kama hizi lazima tumpige mtu bao. Siku hiyo nakwambia lazima tunywe sana, huko Libya kama wao waislam sana si hatuelewi ni masanga mpaka asubuhi.
 
Yule si kipa wa kucheza mashindano yale, nashangaa kwanin kocha hakumpanga dauda huenda angebahatisha kudokonyoa moja. Razack ameimaliza Ghana.

Fainali huwa zina miiko na maandalizi yake...

Leo hii Ivory Coast pengine wanashukuru kwa kipa nambari moja kuwa majeruhi...

Kipa mzoefu ndiye kawaokoa na kawapa ubingwa...
 
Kiukweli Ghana ndo walkuwa wanadeserve zs win....Daa lile goalkeeper lao n kilaza kuwah kutokea kawalet down...
 
Ni nderemo na vifijo kwa wachezaji na mashabiki wa timu ya taifa la Ivory Coast baada ya kufanikiwa kuibwaga timu ya taifa la Ghana kwa mikwaju ya penati 9-8, ni usiku huu ambao unamfanya golikipa wa Ghana kuibuka shujaa, amepangua penati na amefunga
Ha ha ha ha!! Wa kukurupuka
 
Dindane
zakora
Drogba
Eboue
Walistahili kumaliza viwango vyao na hili kombe
 
Kitu ambacho sijakipenda kwenye kombe hili ni kuwa tuna makocha wengi kutoka nje .Mpira wetu hauwezi kuendelea kama hatuamini Ngozi yetu.Iwekwe sheria ya makocha kutoka Afrika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…