Africa Cup of Nations (AFCON) 2015 updates

Africa Cup of Nations (AFCON) 2015 updates

Stars hahaahaaa alichezaga 1980 muda wake ulikuaga huo saivi ni akina cape verde gabon nk
Stars kucheza tena afcon labda 2035
Eeeh ee ee miaka nenda ile, Nasikia walipewa nafasi ile baada ya Somaliya kushindwa kuuhudhuria ?!! (kweli west Afrika wanapiga kabumbu )
 
Refa labda yule aliyechezesha mtani jembe haahaaahaaa

Wanatumia vigezo gani?,naamini tuna marefa wazuri tu,Kama yule aliyechezesha mtani jembe siku ambayo kandambili ilitafunwa,lakini yule wa Jana aliyewabeba Yanga wataishia na kuzeekea kuchezesha ndondo...
 
Eeeh ee ee miaka nenda ile, Nasikia walipewa nafasi ile baada ya Somaliya kushindwa kuuhudhuria ?!! (kweli west Afrika wanapiga kabumbu )

Kumbe na hiyo nafasi tulipewa 1980??
Kiukweli kwa match za jana na team na wachezaji walivyo stars kucheza haya mashindano ni ndoto kbs
 
Wanatumia vigezo gani?,naamini tuna marefa wazuri tu,Kama yule aliyechezesha mtani jembe siku ambayo kandambili ilitafunwa,lakini yule wa Jana aliyewabeba Yanga wataishia na kuzeekea kuchezesha ndondo...

Kifupi ni kwamba Tanzania tuna njia ndefu kufikia maendeleo ya mpira sio wachezaji tu yaani ni kureform wachezaji,makocha,mashabiki, viongozi wa mpira
Yaani zingeundwa hata academy za mashabiki sio wachezaji pekee yake.
 
Kumbe na hiyo nafasi tulipewa 1980??
Kiukweli kwa match za jana na team na wachezaji walivyo stars kucheza haya mashindano ni ndoto kbs
Tutafik one day !!

Tafadhali mkuu ivo unatazama hizo mechi katika mtandao gani au channels / frequencies gani ? niwahi mkuu...
 
Tutafik one day !!

Tafadhali mkuu ivo unatazama hizo mechi katika mtandao gani au channels / frequencies gani ? niwahi mkuu...

Kwa ving'amuzi vya nyumbani
-Startimes wanaonyesha kupitia TBC2
-Azam wanaonyesha kupitia UBC
 
Kifupi ni kwamba Tanzania tuna njia ndefu kufikia maendeleo ya mpira sio wachezaji tu yaani ni kureform wachezaji,makocha,mashabiki, viongozi wa mpira
Yaani zingeundwa hata academy za mashabiki sio wachezaji pekee yake.

Ni kweli mkuu,hapa hatuna mashabiki tuna wehu,timu yake inafungwa,mshabiki anang'oa viti,anaharibu miundombinu mingine ya kiwanja,nashindwa kujua viti ninahusiana vipi na timu yake kufungwa?....tuna safari ndefu Sana...
 
Nashukuru Mungu Tz hatukueza kufuzu katika mashindano hayo maana tungetia aibu mipira unaopigwa kule ni mwingi mno ....
Nilichokiona leo v
Kiwanja kilijaa sijui kwa match zinazofata

Hakika tungetia aibu aiseee!!! manake game nilizoziona jana si mchezo, vijana wanacheza mpira wa nguvu na wa kiufundi wa hali ya juu, nimewaona akina Aubameyang na akina petroipa walivyokuwa wanalisakata kabumbu kwa ustadi, na hizi beki zetu za akina yondani na baba ubaya na osca sijui kama tusingepigwa wiki wiki huko.
 
mkolaj sisi Tz kwenye mipira wa miguu bado sana asee.
 
Last edited by a moderator:
Mmmh! mkuu Mc Tilly Chizenga nilikuwa nimevurugwa sana ile jana baada ya timu ninayoipenda ya wananchi kutoa sare pale taifa dhidi ya wanajeshi wa ruvu shooting. Ila ndo hivo hadi dakika ya 19 Gabon ilikuwa mbele kwa goli la Pierre Aubameyang huyu mchezaji wa Borussia Dotmund-German

Pole sana Mkuu mkolaj
 
Last edited by a moderator:
mkolaj sisi Tz kwenye mipira wa miguu bado sana asee.
Tena sana kwa game nilizoziona jana sijui kama tz inaweza kupambana na hawa wababe tukaambulia kitu, ni hatari congo brazaville walipiga mpira mkubwa mpaka wenyeji wa mashindano wakaomba mpira uishe, manake wangeumbuka nyumbani kwao mbele ya jamaa zao na wakezao,
Sijui leo itakuwaje pale wababe wa congo drc watakapomenyana na chipolopolo ya zambia!!!!!!.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom