Nimekuelewa. Lakini kwa kumalizia tu wazo langu. Hakuna siku TZ au SA au nchi yoyote kubwa itakuja kuwa na mgao wa umeme kwa kila mtu kabla ya nchi ndogo. Yaani kabla ya watu 60 million kupata mgao wa umeme itakuwa ni shida sana. Lakini kugawa umeme kwa watu 1 million ni kazi kidogo sana. Vile vile kujenga lami katika kisiwa kidogo kama Seychelles kila pembe ili kila mwananchi aweze kutumia lami ni kazi kidogo sana ila kujenga lami katika nchi kubwa kama TZ kila pembe ili kila mwananchi atumie lami ni kazi ngumu sana. Kwa hivyo lazima uzingatie pia ukubwa na nchi na ukubwa wa population. Nadhani makosa unayofanya ni kuangalia 20,000 km ya lami ya TZ na kushangaa kwa nini kanchi kadogo kama Seychelles kamewashinda. Ila kama kila mtu Seychelles ana lami nje ya nyumba yake basi mbona Seychelles wasiwe juu yenu hata kama wana 1,000 km ya lami pekee? Hii ndio maana halisi ya per capita na inatumika sana in economics. Hatuzingatii tu 20,000 km yenu na kuilinganisha na 1,000 km ya Seychelles na kusema nyinyi ndio mumeshinda. Hapana. Urefu wa barabara haina maana ikiwa haifikii kila mtu. Hata mkiwa na kilomita milioni moja ya lami na haifikii 20% ya wananchi basi bado mpo nyuma ya Seychelles ambao wananchi wake wote wanaishi karibu na lami.