Africa Kusini haijawahi kuwa na Rais wa kueleweka tena baada ya Nelson Mandela

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Nimeangalia mkutano wa waandishi wa habari kati ya Rais wa Africa Kusini, Cyril Ramaphosa na mwenyeji wake Rais wa Marekani, Trump katika Ikulu ya Marekani nimeishia kumuhurumia na kuisikitikia Africa Kusini.

Ni kama bwana Cyril hakujiandaa au hakuandaliwa kabisa na watu wake kumkabili mwendawazimu Trump. Ramaphosa ameishia kuhangaika kitini, kujikuna kuna, kutetemeka na kucheka cheka tu muda mwingi.

Hivi ni kweli Ramaphosa ameshindwa kuvumilia miaka minne mwendawazimu Trump aondoke madarakani kuliko kujiaibisha na kuiabisha nchi yake hiyo dunia nzima?! Au maslahi yake binafsi ya kibiashara ni makubwa mno kushindwa kuvumilia miaka minne ipite!

Africa Kusini ina bahati mbaya sana tangu Mandela amalize urais, haijawahi kuwa na Raisi wa kueleweka. Kwa mbali Thabo Mbeki alikuwa na akili kiasi na alianza vizuri ila mwishowe akatumbukia kwenye conspiracies za kukataa uwepo wa ugonjwa wa UKIMWI na kugoma kuchukua hatua zozote za kupambana na janga hilo hali iliyopelekea mamilioni ya raia wa Africa Kusini kufa kama kuku wenye mdondo au kideri.

Mrithi wake Jacob Zuma alikuwa ni mtu wa hovyo, asiye na elimu, mpenda ngono na anasa za kila aina na fisadi wa kutupwa aliyeiba fedha za umma na kuikabidhi serikali kwa Wahindi mafisadi waliojitengeneza na kujipakulia tenda za serikali kiholela tu.

Mrithi wa Zuma, Cyril Ramaphosa ambaye ni mfanyabiashara bilionea ameshindwa kufanya chochote kuhusu ufisadi na uhalifu, yupo yupo tu. Chini ya utawala wake ANC imepoteza hadi wingi wa viti bungeni na imebidi kutafuta vyama vingine kuunda serikali. Mkutano wake huko Marekani umedhihirisha muendelezo wa kufilisika kwa ofisi ya urais Africa Kusini. Ni bahati mbaya tu hakuna chama mbadala cha kuirithi ANC nchini humo.
 
Mkuu....japo tunaongea tu Kwa mdomo ila u- raisi ni taasisi ngumu mno .........usidhani huyo ramaphosa kapenda kwenda kwa mwamba trump ujue amebanwa mbavu sehemu [emoji23][emoji23]

Sometimes watawala wanabanwa kwenye Kona [emoji23][emoji23] kiasi Kwamba lazima ukapige goti

Mind u ........ ramaphosa sio Putin [emoji23]

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Ni kama bwana Cyril hakujiandaa au hakuandaliwa kabisa na watu wake kumkabili mwendawazimu Trump. Ramaphosa ameishia kuhangaika kitini, kujikuna kuna na kucheka cheka tu muda mwingi.

Hivi ni kweli Ramaphosa ameshindwa kuvumilia miaka minne mwendawazimu Trump aondoke madarakani kuliko kujiaibisha na kuiabisha nchi yake hiyo dunia nzima?! Au maslahi yake binafsi ya kibiashara ni makubwa mno kushindwa kuvumilia miaka minne ipite!

Africa Kusini ina bahati mbaya sana tangu Mandela amalize urais, haijawahi kuwa na Raisi wa kueleweka. Kwa mbali Thabo Mbeki alikuwa na akili kiasi na alianza vizuri ila mwishowe akatumbukia kwenye conspiracies za kukataa uwepo wa ugonjwa wa UKIMWI na kugoma kuchukua hatua zozote za kupambana na janga hilo hali iliyopelekea mamilioni ya raia wa Africa Kusini kufa kama kuku wenye mdondo au kideri.

Mrithi wake Jacob Zuma alikuwa ni mtu wa hovyo, asiye na elimu, mpenda ngono na anasa za kila aina na fisadi wa kutupwa aliyeiba fedha za umma na kuikabidhi serikali kwa Wahindi mafisadi waliojitengeneza na kujipakulia tenda za serikali kiholela tu.

Mrithi wa Zuma, Cyril Ramaphosa ambaye ni mfanyabiashara bilionea ameshindwa kufanya chochote kuhusu ufisadi na uhalifu, yupo yupo tu. Chini ya utawala wake ANC imepoteza hadi wingi wa viti bungeni na imebidi kutafuta vyama vingine kuunda serikali. Mkutano wake huko Marekani umedhihirisha muendelezo wa kufilisika kwa ofisi ya urais Africa Kusini. Ni bahati mbaya tu hakuna chama mbadala cha kuirithi ANC nchini humo.
Kwamba Thabo alikataa uwepo wa Ukimwi? Mbona kaka yako alikataa uwepo wa Corona? Walikufa wangapi?

Sometimes, watu kama Trump, lazima ujishushe kudeal nao. Cyril ameangalia maslahi mapana ya taifa lake. Kuna millions of people ajira zao zinategemea biashara Kati ya mataifa haya Mawili. Ingawa Trump ni mwehu, lakini angalau kuna mawili matatu biashara za SA zinaweza Salimika.

Ila kweli US kama ni Rais wamepata…..duh…..
 
Mkuu wangu hemu tujikite Gaza kwa sasa achana na ishu za Soweto
 
Mkuu....japo tunaongea tu Kwa mdomo ila u- raisi ni taasisi ngumu mno .........usidhani huyo ramaphosa kapenda kwenda kwa mwamba trump ujue amebanwa mbavu sehemu [emoji23][emoji23]

Sometimes watawala wanabanwa kwenye Kona [emoji23][emoji23] kiasi Kwamba lazima ukapige goti

Mind u ........ ramaphosa sio Putin [emoji23]

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Hajabanwa popote, ni kiherere chake tu.
 
Mandela mwenyewe alifanya nini cha maana zaidi ya kuwasamehe mizungu?
Mandela ni kipenzi cha mizungu sababu aliwasamehe ila hakufanya lolote la msingi SA wala Afrika kwa ujumla. Unakuta mtu tena asiye msouth anamhusudu Mandela hadi kujichora tattoo yake. Ni ajabu na kweli.
 
Nimeangalia mkutano wa waandishi wa habari kati ya Rais wa Africa Kusini, Cyril Ramaphosa na mwenyeji wake Rais wa Marekani, Trump katika Ikulu ya Marekani nimeishia kumuhurumia na kuisikitikia Africa Kusini.

Ni kama bwana Cyril hakujiandaa au hakuandaliwa kabisa na watu wake kumkabili mwendawazimu Trump. Ramaphosa ameishia kuhangaika kitini, kujikuna kuna, kutetemeka na kucheka cheka tu muda mwingi.

Hivi ni kweli Ramaphosa ameshindwa kuvumilia miaka minne mwendawazimu Trump aondoke madarakani kuliko kujiaibisha na kuiabisha nchi yake hiyo dunia nzima?! Au maslahi yake binafsi ya kibiashara ni makubwa mno kushindwa kuvumilia miaka minne ipite!

Africa Kusini ina bahati mbaya sana tangu Mandela amalize urais, haijawahi kuwa na Raisi wa kueleweka. Kwa mbali Thabo Mbeki alikuwa na akili kiasi na alianza vizuri ila mwishowe akatumbukia kwenye conspiracies za kukataa uwepo wa ugonjwa wa UKIMWI na kugoma kuchukua hatua zozote za kupambana na janga hilo hali iliyopelekea mamilioni ya raia wa Africa Kusini kufa kama kuku wenye mdondo au kideri.

Mrithi wake Jacob Zuma alikuwa ni mtu wa hovyo, asiye na elimu, mpenda ngono na anasa za kila aina na fisadi wa kutupwa aliyeiba fedha za umma na kuikabidhi serikali kwa Wahindi mafisadi waliojitengeneza na kujipakulia tenda za serikali kiholela tu.

Mrithi wa Zuma, Cyril Ramaphosa ambaye ni mfanyabiashara bilionea ameshindwa kufanya chochote kuhusu ufisadi na uhalifu, yupo yupo tu. Chini ya utawala wake ANC imepoteza hadi wingi wa viti bungeni na imebidi kutafuta vyama vingine kuunda serikali. Mkutano wake huko Marekani umedhihirisha muendelezo wa kufilisika kwa ofisi ya urais Africa Kusini. Ni bahati mbaya tu hakuna chama mbadala cha kuirithi ANC nchini humo.
Nchi inapenda bia na nyama kuliko akili.

Hapa kwetu tumepata nchi inavisasi vya raisi tokea wajomba zake kufukuzwa mapinduzi.
Kuna lijinga limoja uganda la toto la baba linasifu ila lijajua bila tz basi uganda ingekuwa congo samsung fold
 
Kwamba Thabo alikataa uwepo wa Ukimwi? Mbona kaka yako alikataa uwepo wa Corona? Walikufa wangapi?

Sometimes, watu kama Trump, lazima ujishushe kudeal nao. Cyril ameangalia maslahi mapana ya taifa lake. Kuna millions of people ajira zao zinategemea biashara Kati ya mataifa haya Mawili. Ingawa Trump ni mwehu, lakini angalau kuna mawili matatu biashara za SA zinaweza Salimika.

Ila kweli US kama ni Rais wamepata…..duh…..
Ndiyo, Mbeki alikaata uwepo wa UKIMWI, alikataa UKIMWI kuwa unatokana na HIV na alikuwa anapinga matumizi ya ARVs, jinsi Mbeki alivyouchukulia UKIMWI n
ni kama vile jiwe alivyochukulia Covid.
 
Mandela mwenyewe alifanya nini cha maana zaidi ya kuwasamehe mizungu?
Mandela ni kipenzi cha mizungu sababu aliwasamehe ila hakufanya lolote la msingi SA wala Afrika kwa ujumla. Unakuta mtu tena asiye msouth anamhusudu Mandela hadi kujichora tattoo yake. Ni ajabu na kweli.
Mandela alitoka jela akiwa na miaka 72, nusu ya miaka ya maisha yake akiwa ameitumikia gerezani kusaga kokoto, tayari alikuwa ameshachoka usingeweza kumtegemea afanaye jambo kubwa sana. Hata hivyo kuwasamehe wazungu ilikuwa haiepukiki kwa mustakabali mwema wa Africa Kusini. Hakuna namna yoyote wangweza kufidia madhila kwa kisasi, jambo la muhimu ilikuwa kujenga hadhi na uchumi wa mtu mweusi.
 
Bado hamna cha maana alichofanya so you might as well say SA haijawahi pata rais mweusi wa maana. Wote hamna cha maana walichofanya including Mandela.
 
Nadhani thabo Mbeki ndiye raisi bora ila ni vile tu Waafrika Kusini hawakumpa muda na yeye hakujiandaa na siasa chafu lakini ni bonge la mtu
 
Uk
Nimeangalia mkutano wa waandishi wa habari kati ya Rais wa Africa Kusini, Cyril Ramaphosa na mwenyeji wake Rais wa Marekani, Trump katika Ikulu ya Marekani nimeishia kumuhurumia na kuisikitikia Africa Kusini.

Ni kama bwana Cyril hakujiandaa au hakuandaliwa kabisa na watu wake kumkabili mwendawazimu Trump. Ramaphosa ameishia kuhangaika kitini, kujikuna kuna, kutetemeka na kucheka cheka tu muda mwingi.

Hivi ni kweli Ramaphosa ameshindwa kuvumilia miaka minne mwendawazimu Trump aondoke madarakani kuliko kujiaibisha na kuiabisha nchi yake hiyo dunia nzima?! Au maslahi yake binafsi ya kibiashara ni makubwa mno kushindwa kuvumilia miaka minne ipite!

Africa Kusini ina bahati mbaya sana tangu Mandela amalize urais, haijawahi kuwa na Raisi wa kueleweka. Kwa mbali Thabo Mbeki alikuwa na akili kiasi na alianza vizuri ila mwishowe akatumbukia kwenye conspiracies za kukataa uwepo wa ugonjwa wa UKIMWI na kugoma kuchukua hatua zozote za kupambana na janga hilo hali iliyopelekea mamilioni ya raia wa Africa Kusini kufa kama kuku wenye mdondo au kideri.

Mrithi wake Jacob Zuma alikuwa ni mtu wa hovyo, asiye na elimu, mpenda ngono na anasa za kila aina na fisadi wa kutupwa aliyeiba fedha za umma na kuikabidhi serikali kwa Wahindi mafisadi waliojitengeneza na kujipakulia tenda za serikali kiholela tu.

Mrithi wa Zuma, Cyril Ramaphosa ambaye ni mfanyabiashara bilionea ameshindwa kufanya chochote kuhusu ufisadi na uhalifu, yupo yupo tu. Chini ya utawala wake ANC imepoteza hadi wingi wa viti bungeni na imebidi kutafuta vyama vingine kuunda serikali. Mkutano wake huko Marekani umedhihirisha muendelezo wa kufilisika kwa ofisi ya urais Africa Kusini. Ni bahati mbaya tu hakuna chama mbadala cha kuirithi ANC nchini humo.
Hakuna ugonjwa wa ukimwi,ukimwi si ugonjwa bali ukosefu wa kinga mwilini
 
Bado hamna cha maana alichofanya so you might as well say SA haijawahi pata rais mweusi wa maana. Wote hamna cha maana walichofanya including Mandela.
'cha maana' kinapimwaje?
 
Nadhani thabo Mbeki ndiye raisi bora ila ni vile tu Waafrika Kusini hawakumpa muda na yeye hakujiandaa na siasa chafu lakini ni bonge la mtu
Rais bora aliyepelekea zaidi ya raia wake 300,000 kufa kwa sera ya kukataa matumizi ya ARVs kwa wagonjwa wa UKIMWI na watoto zaidi ya 35,000 kuzaliwa na HIV.
 
Ndiyo, Mbeki alikaata uwepo wa UKIMWI, alikataa UKIMWI kuwa unatokana na HIV na alikuwa anapinga matumizi ya ARVs, jinsi Mbeki alivyouchukulia UKIMWI n
ni kama vile jiwe alivyochukulia Covid.
Sasa na wewe kwa akili yako finyu mpaka sasa bado haujagundua tu na kujifunza kuwa corona ilikuwa ni propaganda za magharibi ili waendelee kututawala mind zetu waafrika na kutuuzia dawa zao
 
Bado sijagundua.
 
Wajinga mpo wengi humu!!
 
Back
Top Bottom