Nimeangalia mkutano wa waandishi wa habari kati ya Rais wa Africa Kusini, Cyril Ramaphosa na mwenyeji wake Rais wa Marekani, Trump katika Ikulu ya Marekani nimeishia kumuhurumia na kuisikitikia Africa Kusini.
Ni kama bwana Cyril hakujiandaa au hakuandaliwa kabisa na watu wake kumkabili mwendawazimu Trump. Ramaphosa ameishia kuhangaika kitini, kujikuna kuna, kutetemeka na kucheka cheka tu muda mwingi.
Hivi ni kweli Ramaphosa ameshindwa kuvumilia miaka minne mwendawazimu Trump aondoke madarakani kuliko kujiaibisha na kuiabisha nchi yake hiyo dunia nzima?! Au maslahi yake binafsi ya kibiashara ni makubwa mno kushindwa kuvumilia miaka minne ipite!
Africa Kusini ina bahati mbaya sana tangu Mandela amalize urais, haijawahi kuwa na Raisi wa kueleweka. Kwa mbali Thabo Mbeki alikuwa na akili kiasi na alianza vizuri ila mwishowe akatumbukia kwenye conspiracies za kukataa uwepo wa ugonjwa wa UKIMWI na kugoma kuchukua hatua zozote za kupambana na janga hilo hali iliyopelekea mamilioni ya raia wa Africa Kusini kufa kama kuku wenye mdondo au kideri.
Mrithi wake Jacob Zuma alikuwa ni mtu wa hovyo, asiye na elimu, mpenda ngono na anasa za kila aina na fisadi wa kutupwa aliyeiba fedha za umma na kuikabidhi serikali kwa Wahindi mafisadi waliojitengeneza na kujipakulia tenda za serikali kiholela tu.
Mrithi wa Zuma, Cyril Ramaphosa ambaye ni mfanyabiashara bilionea ameshindwa kufanya chochote kuhusu ufisadi na uhalifu, yupo yupo tu. Chini ya utawala wake ANC imepoteza hadi wingi wa viti bungeni na imebidi kutafuta vyama vingine kuunda serikali. Mkutano wake huko Marekani umedhihirisha muendelezo wa kufilisika kwa ofisi ya urais Africa Kusini. Ni bahati mbaya tu hakuna chama mbadala cha kuirithi ANC nchini humo.