Umefika hatua hata ukitaka kumsaidia mtu anakuhisi unataka kumtapeli.
Kwa madiba palinishangaza sana, watu wanaishi kwa kuliana Timing, hii inasababisha hata ukitaka kumsaidia mtu anahisi unataka kumtapeli.
Ilikuwa siku moja nipo Johannesburg katika mji wa Germiston, nikamsikia jamaa mmoja anaongea kiswahili fulan japo ilikuwa na lafudhi ya Kenya hivi nikasema mwenzangu huyu hata tupige stori moja mbili tatu za hapa(japo kuwa mimi nilikuwa napita naenda nchi nyingine).
Nilishangaa sana jamaa kaniruka tena kwa maneno ya kunishangaza, mwenyeji wangu nilipomsimulia hii kisa akanambia S. Afrika usimuamini mtu hiyo ni kanuni yakwanza ambayo ni lazima uifate. Kwangu mimi niliona km ni kanuni inayoweza kukunyima fursa mpya maana kuna mwingine atataka akusaidie tuu.