Africa writers series

Africa writers series

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Hawa watu wanapotea kabisa, waliobaki ni wazee wakiwa wanahesabu siku zao tu, lakini wamefanya makubwa mno hasa kwenye upande wa uandishi wenye kufikirisha na fasihi ya ndani mno, maandiko yao yamesaidia sana kuleta ukombozi barani Afrika, lakini pia kuwasaidia waafrika kujielewa na kujitambua hasa wakati wa ukoloni na baada ya uhuru. maandiko yak leo hii yamejaa kwenye vyuo vingi maarufu duniani
kwa sisi tuliobahatika kusoma wakati ule, ambapo mfumo wetu wa elimu ulikuwa haujaparaganyika tulifaidi sana sasa
leo basi ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaenzi hebu tujikumbuke baadhj ya vitabu vyao ambavyo vilihit, kuna vya kiada na kuna vya ziada bila kusahau pia riwaya, nitaanza kwa kutaja baadhi ongezea utakavyokumbuka
CHINUA ACHEBE
-Things fall apart
_No longer at easy
-Okonkwo nk nk
J.K nyerere
Shaaban roberts
Ngugi wa Thiongo
Joram kiango
na wengineo wengi wengi wengi, wameitangaza Afika wakaiweka kwenye ramani ya dunia
karibuni
 
soko la vitabu limekuwa dogo linalochangiwa utamaduni wa sasa wa kutopendelea kusoma vitabu,waandishi wengi siku hizi wapo katika biashara ya siasa,kuandika mazuri ya vyama,,wanasiasa,na serikali huko hulipwa mapesa mengi kuliko vitabu.
 
Natamani kungekuwepo na waandishi waandikao kutokana na mazingira tuliyonayo sasa. Sasa hivi wanakimbilia siasa tu. Hivi kweli hatuna vijana wanaoonesha angalau upeo katika uandishi wao wa riwaya?
 
Nchi isyokuwa na fasihi ni kama maiti aliyeko kaburini.
 
The beautiful ones are not yet born
A man of the people
The river between
Things fall apart
Is it possible
Mine boy
Three suitors one husband
 
Nadhani miaka ya sabini pia nilisoma kimoja kiinaitwa This Day Tomorrow, ila sijkumbukii kiliandikwa na nani; labda Cyprian Ekwensi.
 
Nadhani miaka ya sabini pia nilisoma kimoja kiinaitwa This Day Tomorrow, ila sijkumbukii kiliandikwa na nani; labda Cyprian Ekwensi.
Bila kumsahau nguli mmoja wa malavidavi miaka hiyooooooo anaitwa David G. Maillu. Nyerere alipiga marufuku novels zake.
Moja ya vitabu vyake ni:
My dear bottle
Unfit for human consumption
 
Bila kumsahau nguli mmoja wa malavidavi miaka hiyooooooo anaitwa David G. Maillu. Nyerere alipiga marufuku novels zake.
Moja ya vitabu vyake ni:
My dear bottle
Unfit for human consumption

Ninavifahamu hivyo, nilikuwa navyo kabla havijapigwa marufuku. Kuna mwingine wa Uganda sikumbuki jina lake tena, nadhani lilikuwa na kitu kama Tumusiime. Aliandika jinsi alivyondishwa ku-do majambozi na wasichana angali mdogo sana ambapo mwalimu wake walikuwa msichana mkubwa aliyekuwa akiitwa Matama; kila somo la msichana huyo lilikuwa likiendana na "Practicals." Matokeo yake alipokuwa ofisa mkubwa serikalini akawa hawezi kufanya kazi bila kudu na wafiuasi wake wa kikekiasi kuwa utendaji wake ukawa duni sana. Kilikuwa na mfunzo mengi sana kwa jamii yetu
 
Nchi ya kusadikika
The grain of wheat
The friend of the people
(Drama)an enemy of the people
Penzi kitovu cha uzembe
The trial of dedan kimathi

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
wizard of the crow- wathiong'o new book. Ametumia miaka 20 kukiandika kina page zaidi ya 700.Nikizuri
 
SPARED.....si kumbuki mwandish wake ila story ya kusisimua sana.
 
Natamani kungekuwepo na waandishi waandikao kutokana na mazingira tuliyonayo sasa. Sasa hivi wanakimbilia siasa tu. Hivi kweli hatuna vijana wanaoonesha angalau upeo katika uandishi wao wa riwaya?

Mimi Binafsi Nimejikuta Nikiwa Na Kipaji Hiki, Nilikuwa Naandika Hadithi Toka Darasa La Tatu Mpaka Mwaka 2011 Nikiwa Form Three, Lengo Kuu Ilikuwa Kuwaburudisha Wanadarasa, Nimesimama Kwa Muda Kwani Nataka Nifanye Kazi Kwa Malengo, Wikihii Nimeanza Kuandika Hadithi Ya Nchi Ya Mazonge, Nimejitoa Kifasihi Licha Ya Changamoto Zilizopo Za Soko Na Mtaji. Sikuhizi Watu Wamegeukia Filamu Ambako Kwakweli Kunatapisha Kumejaa Mapenzi Bila Kujali Umli Wa Waigizaji Na Watazamaji, Licha Ya Ukuta Mkubwa Uliogubika Fasihi Andishi Ninamatumaini Makubwa Iwapo Kazi Yangu Itakuwa Nzuri
 
Back
Top Bottom