AfCFTA ni mkataba wa nchi 52 kati ya nchi 55 za Afrika. Zilizosalia ni Tanzania, Benin na Eritrea. Kati ya nchi 52 kwenye mkataba huu zilizo'bid' kuwa makao makuu ni nchi saba, Kenya, Ghana, Ethiopia, Senegal, Madagascar, Swaziland na Egypt. Ghana wamefanikiwa, hongera zao. Nchi za Ghana na Kenya zina uhusiano wa karibu tangu zamani. Nina maswali mawili kwa mleta mada. Ghana wamefanikiwa na nchi sita zilizosalia, Kenya ikiwemo, zikatupiliwa mbali. Ina maana kwamba kwa akili zako nchi zote hizo sita zilizo'bid' lakini zikakosa kufanikiwa 'zimekataliwa'? Pili, inawahusu kivipi kama Tz(hampo kwenye mkataba wa AfCFTA) na makao makuu yenu mliosalia nje ya muungano huu wa Afrika yatakuwa wapi? Tanzania au kwa vibwengo wenzenu Benin na Eritrea?