African Cup of Nations 2008

African Cup of Nations 2008

Kituuuuuz Ghana Wamerekebisha, sasa ni 2 - 2, maskini Ghana walikuwa wanastahiki kufika mbali zaidi ya hapo walipo fika.
 
Nimekupa rekodi zote hata kombe la dunia pia nimeandika, usisahau kuwa sisi hapa tunaongelea kombe la Africa sio la dunia.

Eti wamisri wanafanya uhuni uwanjani, Uhuni gani bwana wee!! kwani hakuna marefarii uwanjani ? marefarii wanajua kanuni za mchezo kuliko mimi na wewe.

sasa wewe unafikiri kuwa timu zingine hazitaki kushinda katika kombe la Africa zinataka kushiriki kwenye world cup tu?

Brother usitudanganye.

acha ukabila ndugu yangu hii sio vita hii ni Sports.

Timu elio shinda ipe haki yake hata kama hauipendi.

Nadhani wewe ungekuwa Refarii wa mechi hiyo baina ya E.Coast na Egypt ungewapa wamisri red card timu nzima.



Hao wachezaji wa Misri wenye uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu mbona hatuwasikii katika ligi za ulaya (UK, Spain, Italy, France and Germany). Tunawaosikia wakitamba katika ligi hizo kutoka Afrika ni wachezaji wa Ghana, Nigeria, Ivory Coast, Mali n.k.

Usiniambie kwamba life style ya huko imewashinda kwa uislamu wao wanaogopa kulishwa mfalme wa meza au akina Wenger, Banitez, Ferguson na wengineo ni wabaguzi hawawataki waarabu. Wamisri wengi waliokwenda kujaribu Ulaya wengi hawakuonyesha kiwango cha kuridhisha. Na hata wale waliopewa nafasi uchezaji wao umekuwa ni wa kukatisha tamaa, je kulikoni?. Kuna mmisri mmoja kama sikosei anaitwa mido anacheza PL alipokewa kwa shangwe kubwa lakini sasa hivi hata mashabiki wa timu yake wanamzomea kwa kushindwa kucheza kwa kiwango alichotegemewa.

http://www.news24.com/News24/Sport/Soccer/0,,2-9-840_2243771,00.html
 
Ghana 4 Ivory coast 2, Ama kweli Ghana imenikosha, Ghana imecheza vizuri sana mechi zote ila mechi ya Camerun tu wachezaji wao 3 maarufu hawakucheza mechi hiyo ndio mana walifungwa mechi hiyo.

Ghana imezishinda timu strong sana kama vile Morroco Ghinia Nigeria na Ivory Coast, nakuhakikishia Ghana ingefika final kombe lingekuwa ni la Ghana.
 
Waheshimiwa vipi matokeo maendeleo ya mechi ya Cameroon na Misri, sioni hapa!
 
Mpira unaanza 1800 CET, so bado kama masaa matatu!


10 minutes to go before the start of the final match. I hope it'll be very entertaining match and no cheating will be allowed by the officials.
 
Away we go, I put my money on Cameron to win whichever way.
 
tunaenda mapumziko hali ikiwa ni mayai kote hadi sasa, hatujui nani ataangua ila inaonesha cameroun wamezidiwa.

lile suali la kuwa misri ni macheater hujiangusha ili wapate penalti nimeliona ila inaonyesha marefa na wao weshalijulia
 
Najaribu kufikiria Stars wangeenda huko! Sipati picha walahi

invisible unaota bila ya kulala rafiki yangu basi alau fumba macho

ss bado tena sana, hata challenge bado seuze hapa.

naam bali limeanza na tupo tukifatilia chochote tutakuwa tukihabarishana
 
naam dakika ya kumi hawa masri wamefanya move moja mbaya kinoma karibu walete hadithi nyengine
 
ndugu yangu mzalendo halisi upo?

unaona waarabu hao wanavyocheza, mwaka huu si mzaha.

hapa wakishinda cameroun basi itakuwa si bure.

maana mafirauni wanaonesha wamekusudia simba kumchezea sharubu
 
sasa mpira nusu uwanja wanashambulia cameroun kama nyuki ila inaonesha cameroun wameroga maana bao halifunguki
 
Mtu wa Pwani nipo- mpira wa Misri upo juu- wapo makini! May be kwa kuwa hawatumii kilevi!

Cameroon wakishinda basi bahati tu! Leo ni Misri!

Wanaweza kuchaza dk 120 then matuta!
 
Back
Top Bottom