African Development Bank yaidhinisha mkopo wa zaidi ya trilioni 1.4 kujenga reli itakayounganisha Burundi na Tanzania

Huyo bibi hizo pesa anazirudisha kwa mshahara wake?
Kupitia diplomasia ya Uchumi na Kupitia kuaminika kwake ndio maana Tanzania imepewa pesa hiyo baada ya kuwa rated vizuri.

Kazi ya Uongozi wa Samia na utazirudiaha wewe Kwa Kodi ila sifa ni za Samia,sawa bwashee?
 
Kupitia diplomasia ya Uchumi na Kupitia kuaminika kwake ndio maana Tanzania imepewa pesa hiyo baada ya kuwa rated vizuri.

Kazi ya Uongozi wa Samia na utazirudiaha wewe Kwa Kodi ila sifa ni za Samia,sawa bwashee?
Ninaelipa ndio nastahili pongezi, huyo mkojani amepewa tu dhamana ya kuwakilisha walipa kodi.
 
EEEeeHEeee, Kagame hawezi kukubali ujinga huo. Ndiyo maana alitaka aunganishe na Mombasa, badala ya Dar!
Najua kama angekuwa ni Kagame shilingi moja isingeibiwa na wapigaji wangeozea ndani.
 

Maneno mengi ya kupamba, lakini nakuhakikishia hata kama mradi utakuja kukamilika, hali za mataifa haya, hakuna cha pekee kitabadilika.

Tulijenga ya TAZARA, Dar hadi Kaprimposhi, zambia. Tukasema itafungua fursa mbalimbali kwanchi zote kusini mwa Afrika. Je, hizo fursa umeziona? Mpaka tumekosa pesa ya kuendeshea, sasa imebidi tuwarudishie Wachina, waliotujengea. Hii ya SGR tutakaposhindwa kuiendesha, sijui tutamrudushia nani!!

Serikali za Afrika zinaendeshwa na watu wenye upeo mdogo sana, wasio na maarifa yoyote, na wanaojifikiria wenyewe na familia zao kuliko mataifa yao, ndiyo maana hakuna mradi ambao huwa unaendeshwa na Serikali, halafu ukafanikiwa. Wala tusitegemee cha pekee hata kwenye hii SGR itakapomalizika. Malori kwa kuwa ni ya watu binafsi ndiyo yataendelea kuwa ndiyo njia kuu ya kusafirishia mizigo. Ni ajeri hiyo pesa ingetumika kujenga bara maalum ya malori toka Dar mpaka Bujumbura Burundi, mpaka DRC ili itumike na malori ya makampuni binafsi.
 
Hiyo Reli kweli itarudisha fedha kweli? Burundi mizigo yake ni kidogo sana.

Mizigo ya Rwanda ni mingi sana.
Kamwe pesa haitarudi. Mkopo utalipwa kutoka kwenye kodi za mishahara ya wafanyakazi na biashara zinazokamliwa kila siku na TRA. Ikishindikana wataenda kukopa WB, halafu wanaenda kulipa Africa Development Bank.
 
Leo kwa mara ya kwanza umeandika ukweli.
Mimi nina matumaini.
Naamini tumefikia ukingoni mwa ndoto hii mbaya ya CCM. Tutaanza ukurasa mpya; hata kama itakuwa ni chini ya CCM iliyojibadilisha; siyo hii iliyo chini ya huyu mama.

Siioni CCM hii ikidumu hata kidogo.
 
KUna faida gani sisi kukupeshwa, kwanini tusikope pamoja na burudi, ili kushare deni?
 
Meli Tunajenga Tanzania na kazi ya ujenzi wa meli Mpya inaendelea na ukarabati wa meli za zamani unaendelea pia.

Nakumbuka Kuna MoU ya Tzn na DRC ya kujenga Barabara na reli Hadi Kisangani na pia kujenga Barabara na reli Hadi Lubumbashi kutokea huku Lake Tanganyika
 
Mimi nina matumaini.
Naamini tumefikia ukingoni mwa ndoto hii mbaya ya CCM. Tutaanza ukurasa mpya; hata kama itakuwa ni chini ya CCM iliyojibadilisha; siyo hii iliyo chini ya huyu mama.

Siioni CCM hii ikidumu hata kidogo.
I concur with you bro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…