Hukuelewa logic yangu ya kutumia neno "nasikia" inahitajika ubongo wako uwe unafanyakazi vizuri ili uelewe nilikuwa na maanisha nini mkuu. Nimeishi na kufanyakazi Nairobi maeneo ya West Land kwa miaka kibao hivyo naijua Kenya na wakenya wenyewe kuliko uzaniavyo mkuu!!
Mkuu hilo neno "Nasikia" lilikuwa swali chokozi!! Kuna uwezekano lugha inakupiga chenga kidogo!Kama kweli umeishi Kenya miaka sita na bado unatumia neno 'naskia' basi utakua na matatizo ya kiaina. Mimi Bongo nimepaishi na kukatiza mikoa mingi na naweza kueleza kuhusu nchi yenu hiyo zaidi ya wengi wenu wazawa.
Ndio maana nikauliza anachomaanisha ni nini? Nchi nzima akimaanisha Dar sawa, akimaanisha grid ya taifa, nimemwambia ni muongo, Simiyu iko kwa grid ya taifa na haukukatika, na Mwingine ameitolea mfano Dodoma na kwingineko pia, haya wewe uliyesoma vizuri na kuielewa, nipe maana nyingine zaidi ya hizo "nchi nzima" alimaanisha nini?
"Nasikia" ni neno linalotumika kuwasilisha hoja pasi kumfunga mtu mdomo, hapa namaanisha atakupa uwanda mpana wa wewe kujieleza huku yeye akiwa tayari analijua jibu liko na ameshakuandalia swali ama hoja nyingine baada ya kujibu hoja.Kama kweli umeishi Kenya miaka sita na bado unatumia neno 'naskia' basi utakua na matatizo ya kiaina. Mimi Bongo nimepaishi na kukatiza mikoa mingi na naweza kueleza kuhusu nchi yenu hiyo zaidi ya wengi wenu wazawa.
Simiyu.Wewe upo simiyu au upo dom?
Simiyu.
Siiombei mambaya Tanzania yangu ila CCM ndiyo chanzo cha mabaya TanzaniaHuwezi ona mkenya akiongea upuuzi wa dizaini hii kuhusu Kenya, instead atakuwa positive na kutoa mapendekezo, ni aibu nyumba unayoishi unaiombea mabaya!