Afrika huu ndio wakati wa kuikuta Ulaya na Marekani Kiuchumi

Afrika huu ndio wakati wa kuikuta Ulaya na Marekani Kiuchumi

Kaa chini utulie Wewe hujui lolote kwenye masuala ya uchumi na historia!
Hivi unaelewa mwaka 1497 Afrika ilikuwa karibu sawa kimaendeleo na ulaya? Ila Mambo yalianza kugeuka miaka ya 1650,s baaada ya propaganda za wazungu?

Hivi unaelewa kuwa mwaka 1750 hadi kufikia 1850 nchi ya uingeleza ilikuwa kinala wa kiuchumi ulimwenguni kote , huku miaka iyo ya 1750 nchi ya Marekani (USA) ikiwa haina kitu chochote mbaya zaidi ikiwa Ni koloni la Mwingereza, ?

Hivi unaelewa janga la ukame la mwaka 1873, pamoja na uvamizi wa Napoleon mwaka wa 1815, magonjwa ya mazao , , migomo ya wafanyakazi ya mwaka 1811, 1850,s pamoja na majanga ya vita ya 1914 yote haya yaliiporomosha uingereza kiuchumi, na Marekani iliyokuwa mtumwa wa uingereza akawa ndo Bwana wa uingereza?

Hivi huelewi kwamba Marekani ilitumia matatizo ya uingereza kujiimarisha kiuchumi na kijamii?


Hivi huelewi kwamba ilitumia mda mfupi sana kuipiku Uingereza na sasa inaitwa Super power?




Kinachokuharibu Ni ile tunaita colonial Legacy, yani unadhani mtu mweusi hapaswi kufanikiwa kumpita mzungu.

Mungu akiendelea kuweka mkono huu ndio wakati wa kutunga sera nzuri za kiuchumi, Ndio wakati wa taifa kuwekeza kwenye tafiti za kisayansi hata kwa kuwaarika waisrael nchini.

Huu ndio wakati wa kusomesha wanafunzi zaidi na kuwafadhili zaidi( maana suala la kupuzia Elimu ndicho pia kitu kiliiponza Uingereza miaka ya 1851) matokeo yake teknolojia ikabakia pale pale (conservative)

Huu ndio wakati wa kulima sana, huu ndio wakati wa kuongeza mishahara kwa wafanyakazi ili kuongeza purchasing power nchini.

Huu ndio wakati wa kuexport zaidi na kupunguza import.

Huu sio wakati wa kulumbana kisiasa, Mimi Ni chadema lakini wakati huu napaswa kuweka uchadema wangu pembeni na kusaport kila chenye tija.

Nawasalimia.
Kweli kabisa Kuna mtu haamini kuwa anaweza chochote. Huu ndio wakati wa taifa kujikusanya bila kujali rangi, chama, kabila Wala dini ya mtu na kutengeneza dira madhubuti isiyotegemea mtu au chama gani wako madarakani, huu ni ule muda wa kuiangalia Tanzania moja dhidi ya mataifa mengine.

Tuachane na gharama za kuhamia Dodoma badala yake tuwape wananchi matrekta walime mashamba makubwa na wavuvi wapewe meli za kisasa wavue tuwauzie waliojifungia majumbani, jamani Mungu atupe nini?
 
Endeleeni kufanya kazi mfe kama kuku.
Unafahamu watu wangapi wanaokufa kwa malaria kwa siku Tanzania? Unafahamu watu wangapi wanaambukizwa malaria kwa siku Tanzania?

Ni Nani anayewafuatilia wagonjwa wa malaria, TB, ajali za bodaboda, maternal deaths kila siku?

Hospitals zetu zimefurika wagonjwa wa malaria makumi kwa maelfu lakini wazungu wametulia tulii wanachapakazi na kutubandika madeni tusiyoweza kuyalipa na kuzinunua bidhaa zetu kwa bei ghafi.
 
Back
Top Bottom