Afrika inalia kilio cha wakoloni wao kwenye Corona

Afrika inalia kilio cha wakoloni wao kwenye Corona

Mkombozi wa afrika juzi kati aliwabembeleza mabeberu wampe mkopo wa tshs tril. 1 Kwa shariti LA kukubali wazazi kurudi shule
Africa haiwezi kufikiria na kutenda vilevile ilivyofikiria na kutenda kwa miaka 60 kupata matokeo tofauti. Kama tunataka ahueni ni lazima tufikirie upya siasa zetu, katiba zetu, mahusiano yetu na wakoloni wetu wa zamani, falsafa zetu, thamani yetu, utu wetu, rasilimali zetu, elimu yetu tunayowapa watoto wetu na sheria zetu.

Haiwezekani kwa miaka 60 Africa kwa pamoja ibaki hivi ilivyo, tegemezi, maskini, na iliyogubikwa na maradhi mengi ya kishenzi kama kipindupindu, upele, mapunye, minyoo, mafunza, kichocho, TB na malaria.

Hii inaonyesha kuwa iko common factor inayowapin down waafrika. CORONA imekuja kutuonyesha dalili za hiyo factor.

Viongozi wa Africa wengi bado wanajiona kuwa hawawezi kuishi kamwe bila kutegemea misaada na mikopo kutoka kwa jamaa zao hawa, hivyo kuwaudhi ni kosa la jinai, kutokuongea lugha yao mbele yao hata kama yuko mzungu mmoja tu mahala hapo ni kosa la jinai, kutokufanya Kama wanavyotaka wao ni kosa la jinai kwetu.

Tulikwishajichagulia kuwa watu weupe ni bora, Wana akili na kila kitu chao Ni kizuri, hata iwe Ni ushoga, kutoa mimba au kula nyama ya mtu.

Africa inashindwa kukemea ushoga kwa sauti moja kwa sababu hizohizo na misaada, mikopo, ubora wa wazungu, nk. Viongozi wetu hawana huruma na waafrika wenzao bali wazungu, wanaiba mali zetu kuwapa wazungu, wanaachia mali zetu kuibiwa na weupe kwa maslahi yao binafsi.

Hivyo ndio Africa, Kila taifa la Africa yapo makabila yanafahamika ambayo wakoloni waliyatumia Kama vibaraka wao wa ndani katika kuidhoofisha Africa baada ya Uhuru. Wakoloni waliyatumia makabila hayo kupitia dini, elimu, scholarships, urafiki wa miji/mikoa yao na miji/majimbo ya mataifa yao, misaada ya moja kwa moja kwenye mikoa na miji ya makabila hayo.
 
Back
Top Bottom