Hivi majuzi, Klabu ya Magari ya Ujerumani ADAC ilitoa ripoti ya utafiti ikionyesha kuwa karibu 60% ya watu waliohojiwa wa Ujerumani wanafikiria kununua magari ya chapa ya China, huku asilimia 72 ya watu wenye umri wa miaka 18 hadi 39 wakipendelea magari hayo. Kuhusu magari ya umeme, asilimia 80% ya waliohojiwa wanapendelea kununua ya chapa ya China. Wameeleza kwamba bei nafuu na teknolojia bora ya ubunifu ni sababu muhimu kwao kufikiria kununua magari ya umeme ya China.
Hata hivyo, wakati ripoti hiyo ilipotolewa, Umoja wa Ulaya ulipitisha azimio la kuongeza ushuru wa forodha dhidi ya magari ya umeme ya China. Hii ina maana kwamba wateja wa Ulaya watalazimika kulipa zaidi kununua magari ya umeme ya China. Hii sio tu imesababisha pingamizi ya China, hatua hii inayopuuza kabisa mahitaji ya watumiaji wa Ulaya pia imepingwa na baadhi ya nchi za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ujerumani na Hungary, pamoja na makampuni ya magari ya Ulaya kama vile Mercedes-Benz na BMW.
Wanaona kuwa hii inaonekana kama ni vita baridi ya kiuchumi, sio tu haitasaidia kuongeza ushindani wa kimataifa wa magari ya Ulaya, lakini pia italeta athari mbaya zaidi, ikiwa ni pamoja na kuzuia jitihada za pamoja za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kama ilivyosemwa katika magazeti ya "Times" ya Uingereza na "Revolt" ya Hispania, Ulaya, ambayo imejiona kama ni kiongozi duniani katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, inawahamasisha wateja wa Ulaya kuhamia kwenye magari ya umeme, wakati huo huo inajaribu kuzuia usambazaji wa magari bora zaidi ya umeme duniani.
Tofauti na Umoja wa Ulaya, ambayo inasema jambo moja na kufanya jingine, Afrika imeonyesha azma yao na hatua za pamoja katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka ya hivi karibuni, na nchi mbalimbali zimetoa sera za kufuta au kupunguza kodi ili kuhimiza maendeleo ya sekta ya magari ya umeme.
Mathalan serikali ya Kenya, ilizindua mpango wa "Usafiri wa Kielektroniki" Septemba mwaka jana, ikilenga kufanikisha zaidi usafiri wa kijani barabarani na kupunguza uchafuzi wa hewa kwa kuendeleza sekta ya vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati safi.
Kwa mujibu wa takwimu, utoaji wa moshi wa magari katika mji mkuu Nairobi unachangia 40% ya vyanzo vya hewa chafu. Hivi sasa, kuanzia mabasi ya uwanja wa ndege, magari binafsi hadi pikipiki, magari ya umeme ya China yamezidi kuwa maarufu miongoni mwa watumiaji wa Kenya.
Kuhusiana na hili, Cleantechnica, chombo cha habari cha nishati safi kinachojulikana duniani, kiliwahi kusema, "Sekta ya magari ya umeme ya China inayoendelea kwa kasi inakuza mabadiliko ya nishati safi barani Afrika.” Viliporipoti juu ya magari ya umeme ya China ambayo yameingia kwenye soko la Afrika, vyombo vya habari vya Marekani vilitumia neno "mapinduzi ya usafiri wa vyombo vya umeme".
Kwa nini magari ya umeme ya China yanapendwa sana katika nchi za Afrika? Kama watumiaji wa Ulaya wanavyosema, magari ya umeme ya China ni nguvu bora zaidi kuliko magari ya Ulaya na Marekani kwa bei yake na teknolojia yake ya ubunifu. Wakati huo huo, kupitia kuingiza teknolojia ya nishati mpya na uzoefu wa China, nchi za Afrika sio tu zinaweza kupunguza utoaji wa hewa chafu, lakini pia kupata fursa mpya za maendeleo ya kisasa yanayoendeshwa na uchumi wa kijani na rafiki kwa mazingira.
Ukweli umethibitisha kuwa ushirikiano wa kunufaishana ndio njia sahihi! Wakati uamuzi mbaya wa Umoja wa Ualaya unapuuza maslahi ya wateja, Afrika inaweza kufurahia faida za teknolojia mpya kwa bei ya chini. Hii sio tu inawanufaisha watu wa kawaida wa Afrika, lakini pia inatoa mchango kutoka Dunia ya Kusini kwenye maendeleo ya kijani duniani.