kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Kimsingi Afrika yote hakuna demokrasia wala haki kama zile zinazotangazwa na nchi za Magharibi tuwe nazo. watu wetu wameishi kwenye hali hiyo hadi sasa bila shida sana. Hivyo ukosefu wa demokrasia kwao sio tatizo kubwa la kufa au kupona kuwa nalo.
Waafrika wanaishi bila shida kwenye mazingira ambayo jamii inashuhudia kuona wanawake hata wasomi kabisa wananyimwa urithi wa wazazi wao na haki ya kumiliki ardhi ya familia. Jamii iko tayari kuona mabinti wao wanakeketwa, kuozwa bila idhini yao, kufungishwa ndoa wangali wadogo kabisa na wakinamama na watoto kupigwa bila kupewa muda wa kusikilizwa. Huko mashuleni na vyuoni pia hakuna demokrasia, utafanya kile utakachoagizwa kufanya na mwalimu na usipofanya utaadhibiwa. Jamii imezoa na haina shida kuuubwa ya ukosefu wa haki na demokrasia.
Wakoloni wanaotamani kurudi tena kututawala kwa mlango wa nyuma wanatuambia hapana, msiishi hivyo, lazima muwe na demokrasia na haki kama zetu huku. Kuna watu wanaona hawa wazungu wanatupenda saaana na kutuonea huruma na kututakia mema. Kumbe wao wana hesabu zao nyuma ya mgongo wamezificha. Na miongoni mwa sababu hizo ni:
1. Haki/demokrasia ni njia mbaya kwa uzalishaji mali kuliko kutumia nguvu/udikteda. Wao walijilimbikizia mali hii waliyonayo sasa kwa kutumia mali za wizi kutoka kwenye makoloni, watumwa bei huria ya bidhaa zao, kufanyisha watu kazi saa nyingi kwa ujira mdogo na kuajili hata watoto. Baada ya kujilimbikizia mali na mitaji ndio haki za binadamu wakazitangaza na kuzikubali.
2. Demokrasia na haki nyingi itasababisha jamii kulumbana, kupigana na kunyang'anyana haki. malumbano haya yatawapunguzia uzalishaji na uimara wa serikali, na wao wataunga mkono upande au pande zote zinazolumbana kwa nyakati tofauti ili kuuza silaha au kuziangusha serikali na kuwa sehemu ya utawala wa serikali mpya. Wakishakuwa sehemu ya utawala wa serikali mpya watakuwa sehemu ya mipango ya nchi na rasilimali za nchi husika, hivyo kuwa wa kwanza kuingia mikataba ya kiuchumi na kiulinzi na kushiri kwenye kuamua nani auziwe nini na nani achimbe nini wapi.
3. Kama malumbano yakiwa makubwa ya kudai haki, serikali tawala zitalazimika kuwa na jeshi kumbwa la kulinda dola lenye silaha za kisasa ambazo watazinunua kutoka kwa wakoloni kwa gharama kubwa, na wapinzani nao hivyohivyo. Kuwa na jeshi kubwa sana kunalifilisi taifa kwakuwa lazima ulihudumie ipasavyo ili lisikupindue.
Dawa pekee ni kuongoza nchi kwa mkono wa chuma dhidi ya wadai demokrasia wanaopewa misaada na wakoloni. Wakati huohuo kuwa na sera nzuri na katili za kubana matumizi ya serikali na kushuhulikia wala rusha na wabadhilifu wa mali za umma ndani ya serikali ili kuhakikisha nchi na wananchi wanafaidi rasilimali za nchi yao.Hata China wanafanya hivi.
Hakuna kucheka na wadai demokrasia za magharibi wakati ndani ya familia zao hakuna demokrasia. Ukicheka nao jamii inazoea fujo, matusi, kejeli, na mapinduzi. Unacheka na watu waliochoma moto hata vituo vya polisi na ofisi za serikali yako?