Afrika itaendelea siku itakapoacha kupewa misaada toka nje

Afrika itaendelea siku itakapoacha kupewa misaada toka nje

bongo dili

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
12,350
Reaction score
25,180
Ukitaka kumfanya mtu kuwa masikini ili umtawale mpe pesa.Ukiona mtu anakupa msaada hakupendi na hataki ujitegemee.

Zamani wazee wa kichaga Mtoto akimaliza darasa la Saba anafukuzwa nyumbani kwa kuambiwa mkataba wako umeisha wa kula na kukaa hapa nyumbani, hii ili wapush wachaga wengi kupambana kwa uchungu na maumivu kwa njia yeyeto hadi wakawa juu.

watoto wao walikuja kuelewa wazee wao baada ya kufanikiwa kimaisha.

Misaada ni tools ya kuzidi kumfanya Muafrika atopee kwenye umasikini.

Wazungu wanawasaidia Waafrika kwa kuwapa pesa na misaada si kwamba ni wema sana au wanawapenda sana waafrika bali ili wazidi kuwa masikini zaidi ili waweze kuwatawala.

Siku ulaya itakapo acha kuipa pesa afrika ndipo afrika itakapoanza kuinuka, wanatumiaa misaada kupush ajenda zao za Siri mfano ushoga, nk.

Kwa kanuni za asili pia wanatumiaa misaada ili kuchukua baraka zetu kupitia kanuni ya ukitoa unabarikiwa zaidi.Atoae upata zaidi kuliko anaepokea.

Wanajua kabisa hizi pesa hazitofika chini zitadakwa juu kwa juu na kurudi kufichwa bank za ulaya na mafisadi,then wananchi ndio watabebeshwa mzigo wa madeni hadi waingie kaburini.

Huwezi pata penzi bila pesa so Africa ni sawa na pisikali kwa ulaya thus wanatutongoza kwa pesa ili watucontrol kwa ajili ya kupush ajenda zao Siri na kuwini raslimali zetu.
 
Ukizoea kuomba hata ufukuzwe kama mbwa na kudhalilishwa bado utarudi kwa kuinamisha kichwa

Waafrika hatujitambui na tumekuwa na tamaduni ya kuombaomba tu
Tunatukanwa kila matusi ila tupo tu hatuna damu

Hatuna tofauti na waombaji wanaozurura siku nzima kuombaomba.

Hao wataomba miaka na miaka mpaka anaoa kwa hela za kuomba, atawapeleka shule watoto kwa hela za kuomba na atajenga kwa kuomba

Hiyo ndio hulka ya masikini anapotaka kuwa masikini maisha

Na nchi masikini hawana tofauti na hao

Mpaka na list inawekwa hadharani kuwa hizi ndio nchi masikini duniani na sisi tuko karibu na mkia kabisa na tunafurahia

Unamkuta Rais anapanda ndege anaenda masafa marefu kwenda kutembeza bakuli
Sasa huyo ana tofauti gani na anaetoka kwake na kuja madukani kuomba?
 
Haya mambo ya kulazimishwa tufirane ili kupunguza idadi ya watu ni huku Africa huwezi Kuta mataifa mengine yanayojitegemea wakalazimishwa,yote haya ni kwa sababu ya kupenda kupewa.
 
Back
Top Bottom