Afrika kama bara tulishashindwa kujikomboa. Wanasiasa wanakimbilia mali na madaraka tu

Afrika kama bara tulishashindwa kujikomboa. Wanasiasa wanakimbilia mali na madaraka tu

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
3,294
Reaction score
4,920
Ukweli ndio huo. Kama bara Africa ilishajifia.

Viongozi wengi wa Africa wameishia kuwa madalali wa mali za Africa kuzipeleka kwa wazungu. Ni nadra kukuta kiongozi wa Africa mzalendo anayewazia nchi yake kufika mbali. Kwenye makaratasi wana hotuba tamu kuliko asali. Kwenye utekelezaji ni wachungu kama sifongo.

Viongozi wa Africa wakiitwa umoja wa Africa kuhutubia wanatoa hotuba kama wameshushwa kutoka mbinguni. Lakini cha ajabu ukirudi kwenye nchi zao hadi leo wananchi wao hawana uhakika wa maji safi na salama ya kunywa.

Wakati viongozi hao wakishindana misafara ya magari ya kifahali na wale wa mataifa yaliyoendelea, wananchi wao wakisema wanaishia kuitwa wahuni wasio na maadili, eti hawajafunzwa na wazazi wao vyema.

Hivi nyie wenzetu hizo tabia za kudalalia mali za nchi zenu ndio tabia njema mliofundishwa na wazazi wenu?

Africa imejifia mapema sana. Vyama vya siasa imekua sehemu ya kupiga ruzuku na kuotea vitambi. Wananchi walipa kodi wako hoi bin taabani. Nchi nyingi za Africa zina zaidi ya miaka 60 ya uhuru lakini ujinga ndio kwanza unazidi kutamalaki.

Tumebakiwa na elimu ile ile ya kuwa matarishi, wabeba bahasha na wavaa tai. Elimu isiyoweza kutengeneza hata panado ya kituliza homa. Elimu isiyoweza hata kwenda kwa masai na kutafiti anawezaje kuishi kwa mitishamba.

Elimu imegeuka chanzo cha mapato. Vijana wanajazwa madarasani bila walimu wala mafunzo ya vitendo. Baada ya miaka mitatu au minne wanapewa makaratasi yana GPA za kutisha na kuambiwa wakajiajiri.

Soma Pia: Bara la Afrika kugombewa kama "kigoli"

Huko kwenye kujiajiri vijana hawana mitaji. Mikopo ya halmashauri wanapewa makada wa vyama. Yaani ni vurugu tafrani. Wakati deni la mataifa mengi ya Africa linakua, umaskini wa watu nao unatamalaki na kuweka makao ya kudumu.

Africa imetanzika na viongozi wake wako wanastarehe America, Ulaya na Asia huko wakila kwa anasa na kusaza.
 
Back
Top Bottom