Afrika Kusini kuuziwa chanjo ya COVID-19 kwa bei ghali mara mbili ya nchi za Ulaya

Afrika Kusini kuuziwa chanjo ya COVID-19 kwa bei ghali mara mbili ya nchi za Ulaya

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Afrika Kusini inatarajiwa kununua dozi za chanjo ya virusi vya corona ya Oxford-AstraZeneca kwa bei mara mbili na nusu zaidi ya nchi nyingi za Ulaya.

Afrika Kusini ndiyo nchi iliyoathirika zaidi na maambukizi ya COVID-19 barani Afrika, inatarajiwa kupokea dozi milioni 1.5 za virusi vya corona mwishoni mwa mwezi huu na mwezi Februari.

Shirika la Habari la AFP lilimnukuu afisa wa ngazi ya juu wa afya nchini Afrika Kusini akisema kuwa dozi ya Corona itaigharimu nchi hiyo dola 5.25 kwa kila dozi, (sawa na Tsh. 12,180), wakati nchi za Umoja wa Ulaya zikinunua dozi hiyohiyo kwa Euro 1.78 (sawa na Tsh 5000), kwa mujibu wa taarifa iliyovujishwa mtandaoni na Waziri wa Ubelgiji mwezi uliopita.

Taarifa hizi zinatia wasiwasi kuhusu uwazi wa nchi tajiri kushirikiana na nchi maskini katika utoaji wa chanjo hii, hasa katika bei na idadi ya chanjo inayotakiwa kutolewa kwa nchi maskini.

Shirika la Afya duniani, WHO, lilitahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea kwa hali hii, ikiyataka mataifa tajiri kutojilimbikizia chanjo ya corona baada ya chanjo inayokidhi mahitaji kugunduliwa.

Afrika Kusini imeagiza dozi zingine milioni 18.5 za chanjo ya AstraZeneca ambazo zinatarajiwa kufika nchini humo kufikia nusu ya kwanza ya mwaka 2021.
 
Hii imesababishwa na mataifa tajiri kununua chanjo nyingi kwa watu wake hali inayosababisha wengine kukosa au kuipata kwa shida, afadhali nchi ya Canada wao walisema watagawa kwa raia wake chanjo ya Corona, itakayobaki wataitoa bure kwa mataifa ya nchi masikini.

Nadhani shirika la Afya duniani lingetoa bei elekezi kwa kila nchi kununua hiyo chanjo, au mamlaka nyingine mfano UN, ila kama soko litaendelea kubaki huria basi kila mfanyabiashara ataitumia hii nafasi kupiga hela, na hapa siwezi kuwalaumu wazungu kwa kutengeneza chanjo, wakulaumiwa na mchina alietuletea hili balaa duniani.
 
Mtoa mada kazungumzia currency mbili tofauti Dollar and Euros. Sijui ukifanya conversion itakuja mara mbili na nusu?
 
Nimeconvert ni kweli ni 2.43 times higher for SA as compared to Europe.
 
Hakuna uhakika kwamba SA ndio nchi ilioathirika sana na Corona kwa Africa wakati nchi nyingine takwimu na upimaji vimejaa magumashi.
 
sisi je? mchina anatuletea lini jamani?? maana chanjo za mabeberu bei hatutaiweza kwa kweli
 
sisi je? mchina anatuletea lini jamani?? maana chanjo za mabeberu bei hatutaiweza kwa kweli
Watuletee nini! For what!? Labda watuletee fidia ya madini & rasilimali zetu walizokwepua.
 
ina maana africa hakuna watafiti watakaoweza kutengeneza chanjo wakati kila mwaka wanamwagika graduates waliobobea kwenye maswala ya afya?

au walikuwa wanafanya ngono tu huko vyuoni na kukaririr ili wapate ufaulu mkubwa tu ili wakagawe panado?

well tatizo sio watafiti tu bali tatizo ni serikali yao pia sababu hata wanaoendesha serikali ndio haohao graduates.
no hard feelings lakini huo ndio ukweli.

Hakuna pakutokea hapo wote wamejaa kwenye mkono wa mzungu.
 
Hakuna uhakika kwamba SA ndio nchi ilioathirika sana na Corona kwa Africa wakati nchi nyingine takwimu na upimaji vimejaa magumashi.
Km takwimu za upimaji zimejaa magumashi angalia ufaji wao huko hakunaga magumash
 
ina maana africa hakuna watafiti watakaoweza kutengeneza chanjo wakati kila mwaka wanamwagika graduates waliobobea kwenye maswala ya afya?

au walikuwa wanafanya ngono tu huko vyuoni na kukaririr ili wapate ufaulu mkubwa tu ili wakagawe panado?

well tatizo sio watafiti tu bali tatizo ni serikali yao pia sababu hata wanaoendesha serikali ndio haohao graduates.
no hard feelings lakini huo ndio ukweli.

Hakuna pakutokea hapo wote wamejaa kwenye mkono wa mzungu.
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 ngono sio
 
Hii imesababishwa na mataifa tajiri kununua chanjo nyingi kwa watu wake hali inayosababisha wengine kukosa au kuipata kwa shida, afadhali nchi ya Canada wao walisema watagawa kwa raia wake chanjo ya Corona, itakayobaki wataitoa bure kwa mataifa ya nchi masikini.

Nadhani shirika la Afya duniani lingetoa bei elekezi kwa kila nchi kununua hiyo chanjo, au mamlaka nyingine mfano UN, ila kama sok

Mambo mengine tuwe tunaya tafakari kwa kina kabla ya kuanza kulahumu - hatuja wahi kusikia WHO ikishutumu Uchina kwamba Taifa hili ndio chanzo cha ugonjwa wa COVID-19, sikuwahi kusikia Mataifa ya Ulaya yakilahumu Uchina - kampeini za kuisema vibaya China zilianzishwa na Trump pamoja na Pompeo, na kusema ukweli ni Mataifa machache yaliyo kuwa yanaunga mkono madai ya Serikali ya Merikani iliyo pita - kwa kuwa wana sayansi walijua kwamba ungonjwa huu ilianzia huko Merikani mapema zaidi kabla ya Uchina wenyewe walidai eti ni mafua makali watu walikufa wengi tu, lakini baadae wana sayansi walipo fukuwa maiti na kuzifanyia uchungi wa kina zikagundulika walifariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19 na sio mafua makali kama walivyo kuwa wanadai mwanzo.

Wachina walitambuwa tangu mwanzo kwamba ugonjwa huo ulikuwa imported from somewhere to ruin Chinese economy by killing millions of her citizens - ndio maana China haikulaza damu wakafanya kazi usiku na mchana kudhibiti ugonjwa huu hatari na wamefanikiwa.

Siku moja Trump na Pompeo walipo kuwa wana wasema sema vibaya wachina kuhusu gonjwa hili - Rais wa China alikasirika mpaka Waziri wake wa masuala ya nje akalazimika kulitolea ufafanuzi wa kina suala hilo, Trump na Pompeo walikaa kimya kabisa na tangu siku hiyo Trump hakurudia tena kusema kwamba COVID-19 ni virusi vya Kichina, alijuwa wahusika wakuu wa janga hiki ni akina nani.
 
Hakuna uhakika kwamba SA ndio nchi ilioathirika sana na Corona kwa Africa wakati nchi nyingine takwimu na upimaji vimejaa magumashi.
Mkuu, nilipo muona Ramaphosa anasalimiana na Bill Gates kwa bashasha kubwa nukajua kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia - wala sishangazwi chanjo hizo kununuliwa kwa bei lukuki ukilinganisha na bei wanazo nunulia chanjo Mataifa ya magharibi ambazo ni nafuu wakati chanjo ni zile zile.

Kila mara nawakumbusheni kwamba Big Pharma Companies zinazo fadhiliwa na funds za Bill&Melisa Gates foundation ie zina mkono wa Bill Gates, mikono yake imesabaa kwenye taasisi za kimatabibu,maabara za utafiti wa kibailojia na kikemikali mikono yake imesambaa kila sehemu nyeti inafanana kama ya octopus, we fikiria kajiondoa kabisa kutoka kwenye masuala ya ICT ambayo ni fani yake, badala yake kakimbilia kwenye fani nyingine kabisa akiwa na lengo la kutekeleza hidden ajenda zake za muda mrefu, ambazo ntazifafanua hapa chini:

Ya kwanza - yeye na makampuni anayo yafadhili wamejizatiti kupiga hela ndefu kwa kuwa wanajua gonjwa hili ni pandemic hivyo hakuna ujanja watu wote Duniani watalazimika kudungwa chanjo utake husitake, hapo ndipo watakapo tukamatia, hilo la kwanza.

Ya pili, ambayo kwa Bill Gates ndio yenye umuhimu zaidi na anaichangamkia fulsa hii ya kuchonga kwa kuwa anajua lengo lake la muda mrefu la ku-depopulate baadhi ya Mataifa kwa kupitia chanjo ambazo ziko-customised kulenga makontinent fulani basi hilo likitekelezeka malengo yake yatakuwa yametimia.

Watu wengine wanafikiri tunamzulia Bill Gates, hiyo si kweli hata kidogo, mwanadamu huyu hafai hata kidogo, fatilieni/someni historia yake ikiwemo imani yake kuhusu ongezeko la idadi ya binadamu Duniani- hapendi kabisa watu wa Dunia ya tatu kuzaana zaana ovyo na ili halifichi, analisema hata kwenye makongamano - hivyo yeye na mabilionea wenzake wenye akili fyatu kama yeye wanaona wana wajibu mkubwa kutoka kwa sijui mwenyezi Mungu au Lucifer kupunguza idadi ya watu kwenye Mataifa ya Dunia ya tatu ili walinde rasili mali ya Dunia sizije zikatoweka yuko serious kuhusu suala hilo - sasa binadamu wa design kama za Bill Gates wako WIRED vipi kama sio kwamba akili zao hazina tofauti na akili za akina Dracula, Fu Manchu na Frankenstein!
 
Hakuna uhakika kwamba SA ndio nchi ilioathirika sana na Corona kwa Africa wakati nchi nyingine takwimu na upimaji vimejaa magumashi.
Hizo nchi zengine wenyewe wanajua hapa corona imeongezeka tena kwa kiwango gani na ikipungua wanajua bila takwimu,mfano wa hizo nchi ni Tanzania ambayo wenyewe wanasema sasa hivi corona imeongezeka maana kuna muda ilipungua.
 
Back
Top Bottom