Afrika kusini wamtengenezea Brenda Fassie Sanamu ili kumuenzi, Tanzania inaweza kumtendea Msanii gani jambo hili?

Hivi sign official ya kumuenzi Mwalimu Nyerere ni ipi?
 
Juma Kilaza
Aiseee! Umenikumbusha mbali sana, Juma Kilaza jirani yangu wa zamani pale Mt. Fire, Opp na Mashine ya Nafaka kwa wauza Mchele! Kiukweli alikuwa anajua lakini sidhani kama anafikia level za akina Salum Abdallah, Mbaraka Mwinshehe!
 
Aiseee! Umenikumbusha mbali sana, Juma Kilaza jirani yangu wa zamani pale Mt. Fire, Opp na Mashine ya Nafaka kwa wauza Mchele! Kiukweli alikuwa anajua lakini sidhani kama anafikia level za akina Salum Abdallah, Mbaraka Mwinshehe!
Shkamoo mhenga
 
Mkuu wangetutengenezea sanamu la KALI P yule jamaa alikuwa anaimba kama polisi hivi.Aisee nilikuwa namkubali sana maana alisaidia sana jeshi la polisi kujulikana

(Abdul Miraj) Au Kali P! Aliacha Muziki akiwa na Albam ya 3 mkononi bila ya kuipeleka popote! Amekuwa mtu wa dini sana, "tabligh" flani amazing! Ana Mji wake Kitunda, siku hizi hapendi ngoma zake zipigwe, nadhani hilo la sanamu ndio kabisa!
 
Hebu sikiliza Mbiliabel, Yvonne Chakachaka nyimbo zao hata ukiweka msibani watu watatikisa vichwa...

Lazima tukubali starehe na vitu vizuri vilikuwa zamani sio sasa.

Mkuu siku hizi wanatunga ili kupata hela, hawaangalii mbali. Wanatunga wanaweka maneno kadhaa ila maudhui yao yanakuwa madogo sana, tofauti na zamani. Nyimbo nyingi zamani zilikuwa ni burudani na kufundisha
 
Sema mimi kura yangu siku zote inaangukia kwa Marijani, ingawa namuelewa sana Mwinshehe.
Mwishehe alikuwa na sauti tamu sana kusikiliza Marijan alikuwa na mashairi kuntu (alikuwa anajua sana mziki)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…