Afrika Kusini yaahidi kukomesha mashambulizi ya kibaguzi nchini humo

Afrika Kusini yaahidi kukomesha mashambulizi ya kibaguzi nchini humo

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Mamlaka nchini Afrika Kusini siku ya Ijumaa zimeahidi kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohusika na mashambulizi ya kibaguzi (xenophobia) dhidi ya Waghana na raia wengine wa kigeni. Hatua hii inakuja siku moja tu baada ya Ghana kulalamika vikali kufuatia kusambaa kwa video za matukio ya kikatili kwenye mitandao ya kijamii.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa, alimuita balozi wa Afrika Kusini nchini humo siku ya Alhamisi na kuitaka serikali yake iingilie kati haraka "ili kuzuia hali hiyo isizidi kuwa mbaya."

Kwa upande wao, watetezi wa haki za wahamiaji wanasema kuwa raia wa kigeni wamekuwa wakifanywa "mbuzi wa kafara" na kubebeshwa lawama kutokana na ugumu wa maisha na kudorora kwa uchumi nchini Afrika Kusini.

Kupitia mtandao wa X, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ghana ilieleza kusikitishwa kwake na tukio moja lililotokea kwenye jimbo la KwaZulu-Natal. Kwenye tukio hilo, raia mmoja wa Ghana alivamiwa, akatakiwa kuonyesha vibali vinavyomruhusu kuishi nchini humo kisheria, kisha akaambiwa aondoke na arudi "akaitengeneze nchi yake."

Katika kujibu mapigo, Wizara ya Polisi ya Afrika Kusini imetoa tamko kuwa watu wote watakaobainika kushiriki au kuchochea vitendo hivyo vya kibaguzi watasakwa, watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

"Vitendo vya uvunjifu wa sheria, vitisho, na ukatili dhidi ya jamii za wahamiaji havina nafasi katika demokrasia yetu inayoongozwa na katiba," alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, wakati wa kikao na maafisa wa serikali.

Waziri Lamola aliongeza kuwa ukatili dhidi ya wageni ni tishio kubwa kwa utaratibu wa kikatiba wa nchi hiyo. Vilevile, jeshi la polisi limewaomba viongozi wa kijamii na asasi za kiraia kushirikiana nao ili kuzuia mashambulizi zaidi na kuhamasisha utatuzi wa changamoto kupitia mazungumzo.

Kupitia mtandao wa X, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ghana ilieleza kusikitishwa kwake na tukio moja lililotokea kwenye jimbo la KwaZulu-Natal. Kwenye tukio hilo, raia mmoja wa Ghana alivamiwa, akatakiwa kuonyesha vibali vinavyomruhusu kuishi nchini humo kisheria, kisha akaambiwa aondoke na arudi "akaitengeneze nchi yake."

SOURCE: BBC​
 
Kila nchi ikiwajibika ipasavyo kwenye kuleta fursa za maendeleo,hakuna kijana itathubutu kwenda nchi nyingine kubahatisha maisha labda kuwe na fursa zaidi ya ile aliyo nayo, maana yake ataenda kwa lengo la kukuza mtaji wake.
Wazansi waendelee kuwafukuza na kuwachamba wahamiaji ili viongozi wa nchi zao waone aibu.
 
Hawa ni waongo! Wanajikosha tu kwa kuona aibu! Haya matukio hayajaanza mwaka huu, na hufanyika hadharani mbele ya vyombo vya ulinzi na usalama! Wangekuwa na nia ya dhati wangeyakomesha miaka mingi iliyopita!
Wameshasahau maumivu ya kubaguliwa na wazungu!! wakaamua kuwabagua waafrika wenzao! Hii dunia ni yetu sote!! Watumie utaratibu wa kufuata sheria. Aliyeingia nchini mwao kinyume cha sheria wampeleke mahakamani! Au waseme rasmi kuwa ni marufuku waafrika wengine kwenda Afrika ya kusini!!
 
Back
Top Bottom