Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
#CoronaVirus inatarajiwa kuzisukuma nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara katika mporomoko wa kiuchumi mwaka 2020 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25
Ripoti ya Benki ya Dunia kuhusu hali ya kiuchumi barani Afrika imesema uchumi wa bara hilo utashuka kwa asilimia 2.1 na kufikia asilimia 5.1 kutoka kiwango cha ukuaji cha mwaka jana cha asilimia 2.4.
Aidha mripuko huu wa virusi vya Corona utazigharimu nchi za ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika dola bilioni 37 hadi dola bilioni 79 ambayo ni hasara itakayoonekana mwaka huu kufuatia kuvurugwa kwa shughuli nyingi za kibiashara na kiuchumi miongoni mwa sababu nyinginezo.
Bara la Afrika lina alau visa 10,956 vya watu waliothibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, vifo 562 na waliopona wakiwa ni 1,149 kwa mujibu wa takwimu za Shirika la habari la Reuters kwa kuzingatia taarifa zilizokwishatolewa na serikali na data za shirika la Afya Ulimwenguni – WHO.