Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Afrika tumepoteza utamaduni wetu. Rais ni alama ya nchi, madam Rais angevaa vazi la asili la Ethiopia angeweza kuitangaza nchi yake zaidi.
Nikiwa shule ya msingi , Waziri Mkuu wa India, Bi Indira Ghandi (RIP) alitembelea Tanzania akiwa ndani ya vazi la Sari. Sijawahi kumuona mama huyu enzi za uhai wake akiwa nje ya vazi la Sari.
Mbali na kupoteza utamaduni wetu, pia tunanufaisha makampuni ya Magharibi. Usishangae gauni la Madam Rais kuwa ni brand ya Chanel na lilimgharimu US$ 2,000 (Sina uhakika na hili).
Ninawasifu wa Afrika Magharibi, wameamua kufanya kitenge kuwa vazi la asili. Nilishaweka historia ya vitenge hapa. Ni vazi Wa Dutch waliiga Indonesia wakati wana tawala. Waindonesia walipogoma kununua kopi ya vazi lao iliyotengenezwa na Mdutch, soko lilitafutwa Afrika.
Nguo ya asili ya Ethiopia.