Afrika tunaweza kufaidika vipi na vita ya Ukraine?

eliakeem

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Posts
17,214
Reaction score
15,853
Ushabiki tuache kando. Ambao kamwe hautatusaidia kupiga hatua mbele toka hapa tulipo.

Tukiwa kama bara tuna mikakati gani ya kufaidika au kujifunza kutokana na huu mzozo?

Tukiangalia kwenye kilimo biashara nk.

Binafsi naiona fursa kwenye mzozo huu. Tunapaswa kufanya kitu fulani ili kuwa na mkakati.
 
Nina wasi wasi kama hata wakuu wetu wakikaa AU, wanajenga mikakati ya kujifunza hali na kung'amua fursa ambazo zitalinufaisha bara la Afrika.
 
Ccm wao wanapiga akili namna gani wataiba kura 2025 ili huyu mama atawale hadi 2030 nyie mnawaza namna gani tunaweza kufaidika na vita kati ya Ukraine na Russia.
 
Mimi sita liongelea bara la zima Afrika bali nita iongelea zaidi nchi yangu pendwa Tanzania:-
1. Kilimo
- serikali inapaswa kubuni sera mpya zilizo bora zitakazo inufaisha Tanzania kwa asilimia kubwa ili taifa letu lipunguze utegemezi wa baadhi ya bidhaa za shambani[ mazao ] kuagizwa kutoka nje bali tuanze kuyapata hapa hapa nchi na sisi kuyauza nje tukianza kuuza mwanzo kwa Africa mashariki kwanza baadae kufuata Kati, Kusini , Magharibi na bara zima la Afrika mfano mazao Kama mchikichi, Ngano n.k tunapaswa kubuni sera zitakazo tuletea matunda Kama vile :-

i, Kulifanya bara zima la Afrika kututegemea sisi Tanzania kwa bidhaa za shambani [ mazao ] kwa asilimia zaidi 90% ya mazao mbalimbali. Tanzania kuwa “SHAMBA LA AFRIKA”

ii, Serikali kuweka sera bora za kukalibisha wawekezaji wa viwanda vya kuzalisha vifaa vya mashambani ambavyo vitauzwa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania hasa hasa Afrika tuifanye nchi yetu kuwa kiwanda cha Afrika na Dunia cha vifaa vya mashambani mfano Taiwan ni kiwanda cha dunia Cha “Chips”.

iii, Serikali kuweka sera bora zitakazo ifanya serikali kulibeba jukumu la ufanyaji wa tafiti mbalimbali na ufunguaji wa vyuo na viwanda vitakavyo kuwa na kazi ya utafiti na uzalishaji wa mbolea itayao endana na ardhi yetu ya hapa Afrika itakayo Leta matokeo chanya katika kilimo cha kisasa na sio mbolea mbalimbali tunazo agiza kutoka nje ambazo nyingine huleta matokeo hasi kwenye mazao. Tunapaswa kuifanya Tanzania kuwa “kiwanda cha mbolea Cha Afrika”.

iv, Serikali kupitia wizara ya Mambo ya nje inapaswa kujiunganisha Tanzania na wawekezaji mbalimbali wabobevu katika maswala ya kilimo kuja kuwekeza katika ardhi yetu kwa pande zote mbili kunufaika huku sera mbalimbali za uwekezaji katika kilimo zikipaswa kuwa bora zisizo athiri uwekezaji katika sekta ya kilimo.

v, Wizara ya Kilimo inapaswa kutengwa peke yake kwa manufaa zaidi yaani Wizara ya Kilimo inapaswa kujitegemea pekee take pasipo kujuishwa na kitu kingine.

Vi, Serikali inapaswa kuongeza juhudi katika ufundi shaji na utoaji wa elimu ya kilimo cha kisasa katika ngazi mbalimbali ikiwemo mashuleni [ kuanzia elimu ya msingi mpaka Chuo kikuu ] na pia kwenye jamii.
 
Haya yanaweza kutumika kwa bara zima la Afrika.
 
Back
Top Bottom